TUBORESHE MAKAZI KUPUNGUZA UKATILI KATIKA JAMII: DK. JINGU - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday 23 November 2020

TUBORESHE MAKAZI KUPUNGUZA UKATILI KATIKA JAMII: DK. JINGU

Katibu Mkuu Wizara ya Afya - Idara Kuu ya Maendelo ya Jamii Dkt. John Jingu akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Ilalangulu katika Halmashauri ya Mpwimbwe wakati wa Kampeni ya Kuboresha Makazi yenye kauli mbiu ya “Piga Kazi Boresha Makazi”.

Na Mwandishi Wetu, Katavi

KATIBU Mkuu Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendelo ya Jamii Dk. John Jingu amesema ujezi wa nyumba bora katika jamii utasaidia wananchi kuwa na makazi bora na kuondokana na vitendo vya ukatili ambavyo wakati mwingine huanzia katika ngazi ya familia.

 Dk. Jingu ameyasema hayo katka kijiji cha Ilalangulu kilichopo katika Halmshauri ya Mpwimbwe Mkoani Katavi wakati akihamasisha Kampeni ya kuboresha Makazi inayoendelea katika mikoa mbalimbali nchini.

Amesema Wizara inatekeleza mipango ya maendeleo ambayo imepewa kipaumbele katika Ilani ya CCM yam waka 2020-2025 ambayo imeweka wazi umuhimu wa makazi bora kwa taifa lenye afya.

“Wizara inahamashisha wananchi kuboresha makazi yao kwa kujiunga katika vikundi ili kupata mikopo itakayowawezesha kuboresha makazi”.

Ameongeza kuwa kuwa na makazi bora ni maendeleo ya jamii kwani makazi bora yanasaidia familia kuwa na Amani na utulivu katika ustawi wao kwa ujumla.

“Ukiwa hauna nyumba bora unakaribisha wageni wengine kama mende, kunguni, panya na wadudu hatarishi kagtika makazi wanaoondoa amani katika familia,” alisema.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpwimbwe Godfrey Nkuba amesema Halmashauri hiyo imefika asilimia 70 ya makazi bora katika vijiji na Kata zilizopo.

“Vijiji vya Kibaoni na Ilalangulu vinaongoza kwa kuwa na makazi bora na wananchi wamehamasika zaidi katika kub oresha makazi yao,” alisema.

Naye mmoja wa wananchi aliyeboresha makazi yake kwa kutumia kipato chake na mikopo cha vikundi Elizabeth Nyanda amesema kuwa mpango wa Taifa wa kunusuru kaya masikini (TASAF) umemsaidia kupata mtaji wa biashara iliyomuwezesha kujenga nyumba mbili za kisasa na kutoka katika nyumba ya tope na nyasi.

“Namshukuru Rais John Pombe Magufuli na watu wa TASAF kwa kuniwezesha kwa kweli wameniwezesha na wamenikwamua kutoka katika makazi duni,” alisema.

Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii inaendesha Kampeni maalum ya kuhamasisha jamii kuboresha makazi yao ikiwa na kauli mbiu isemayo: “Piga Kazi Boresha Makazi”.

No comments:

Post a Comment