Simu zote hizi zinasubiri washindi ambao ni wateja wote wa Tigo, wauzaji wa jumla wa bidhaa za Tigo, Mawakala, Viongozi wa timu za mauzo, na watoa huduma wakubwa wa huduma za Tigo pesa.
Akizungumza wakati wa kukabidhi simu janja kwa washindi, Meneja wa Tigo, kitengo cha Bidhaa, Suleiman Bushagama, amesema, “Tangu tuzindue kampeni hii, tumetoa zawadi ya dakika za muda wa maongezi zaidi ya milioni 149, MB za data milioni 504 na SMS milioni 81 kwa wateja wetu nchi nzima ambao walinunua vifurushi tangu kuzinduliwa kwa kampeni hii. Leo hii tunakabidhi simu janja kwa washindi wa kila siku na wiki”.

Frank Lyakurwa ambaye,ni mstaafu, kutoka Madale, Dar es Salaam, amejishindia simu janja ya Samsung Note 20 na amefurahi sana baada ya kuibuka mshindi. “Nilinunua bando la internet la wiki kwa shilingi 3,000 ambapo nilipewa bonus ya GB 2, baada ya hapo nilipigiwa simu kwamba nimejishindia Samsung Note 20. Sikuamini,” amesema.
“Nimefurahi sana,” amesema Jorum Mwakipesile kutoka Shinyaanga baada ya kujishindia simu janja ya Itel T20. “Kama ilivyo ada yangu, nilinunua bando la siku la shilingi 500 na kupata ofa ya dakika 10 za muda wa maongezi kwenda mitandao yote. Pia nilifahamishwa kwamba nimejishindia simu ya Itel T20, hii itanisaidia sana kusukuma mbele gurudumu la maisha,” amesema kwa furaha.

Pia washindi wa simu janja wa kila siku pamoja na wiki watapigiwa simu na mfanyakazi wa Tigo kupitia namba maalumu ya kampuni mara tu baada ya droo hizo kufanyika. Ofa hii ni bure, washindi hawapaswi kutoa malipo ya aina yoyote ili kupata zawadi zao. Wateja wote wa Tigo wanashiriki katika ofa hii.
No comments:
Post a Comment