Na Mwandishi Wetu
WAKATI nchi ikiwa inaelekea kwenye Maadhimisho ya kimataifa ya siku16 za kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto takwimu zinaonesho kuwepo kwa ongezeka la matukio ya ukatili huo ambapo ongezeko hilo linatokana na jamii kuwa na uelewa zaidi juu ya madhara yatokanayo na ukatili wa kijinsia na kutoa taarifa za matukio ya ukatili huo katika madawati ya jinsia.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam juu ya uzinduzi wa maadhimisho hayo utakayofanyika 25 mwezi huu Mkuu wa Mawasiliano ya Serikali Wizara ya Afya Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto amesema Serikali imejidhatiti katika kuhakikisha vitendo vya kikatili vinatokomezwa na kutokomezwa kabisa katika jamii za watanzania.
Prudence Costantine amesema katika kuzuia na kutokomeza Vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto Serikali imeanzisha madawati ya jinsia na watoto katika vituo vya Polisi ambapo hadi sasa madawati 420 yameanzishwa na yanafanya kazi kwa Lengo la kuwawezesha wahanga kupata huduma stahiki katika vituo vya Polisi na kutendewa haki.
Aidha Bw. Prudence amesema matukio mbalimbali yatafanyika katika siku 16 za Kupinga Ukatili wa kijinsia ikiwemo utoaji wa elimu juu ya namna ya kupambana na vitendo vya kikatili kupita katika misafara ya Kijinsia itakayojikita katika Vyuo vya Elimu ya Juu na Vyuo vya kati nchini ikiwa ni mpja ya namna ya kupambana na vitendo hivyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Jinsia Grace Mwangwa ameeleza kwamba Serikali inajipanga kuongeza vituo vya kuripoti matukio ya ukatili ili kuhakikisha matukio hayo yanapungua kasi ya kuongezeka ndani ya jamii.
Kwa upande wake Mkururgenzi wa Mtandao wa kutokomeza ukatili kwa wanawake-WILDAF Anna Kulaya amesema Shirika lake linashirikiana na Serikali katika kupambana na kutokomeza kwa kushriki katika jitihada za utoaji elimu kwa wananchi hasa wa vijijini kuhusu namna ya kutokomeza vitendo vya kikatili.
Naye Mkurugenzi wa Shirika la Msaada wa Kisheria -LSF Lulu Ng’wanakilala amesema Shirika lake kwa kushirikiana na Serikali limejikita katika klutoa masaada wa kisheriakwa wahanga wa vitendo vya kikatili ili kuhakikisha wanapata haki na watedaji wa vitendo hivyo wananchukuliwa hatua za kisheria.
Kampeni ya Siku 16 za Kupinga Ukatili zitazinduliwa tarehe 25 Oktoba jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara yav Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu.
No comments:
Post a Comment