NMB YATOA VIFAA VYA AFYA IRINGA, KAGERA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya

Saturday 31 October 2020

NMB YATOA VIFAA VYA AFYA IRINGA, KAGERA

Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja wa NMB - Abella Tarimo (mwenye rasta) akikabidhi sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Iringa (kushoto kwake) Dk. Robert Salim na Mganga Mfawidhi Dk. Alfred Mwakalebela (kulia).

KATIKA
kuadhimisha mwezi wa huduma kwa wateja, Benki ya NMB kupitia Mameneja wake wa huduma kwa wateja wa Kanda ya Dar es Salaam, Nyanda za Juu na Kanda ya Ziwa imetoa vifaa mbalimbali vya Afya vyenye thamani ya sh. milioni Tisa, katika mikoa ya Iringa na Kagera ikiwa ni sehemu ya kurudusha kwa jamii.

Mbali na vifaa hivyo, wafanyakazi wa NMB Tawi la Iringa wametoa vifaa vya shule kwa wanafunzi wa shule za msingi Mapinduzi, Wilolesi na Saint Dominic na baadae kuwapa wanafunzi wa shule hizo elimu juu ya masuala ya kifedha.

 Katika Mkoa wa Iringa, vifaa vilivyokabidhiwa kwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ni; mashuka, vitanda vya kujifungulia kwa akina mama, na vitu mbalimbali kama pampasi, mafuta ya kujipak na sabuni kwa ajili ya watoto.

Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja wa NMB - Abella Tarimo (mwenye rasta) akikabidhi sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Iringa (kushoto kwake) Dk. Robert Salim na Mganga Mfawidhi Dk. Alfred Mwakalebela (kulia).

No comments:

Post a Comment