WAZIRI MUSSA ZUNGU ATEMBELEA BANDA LA BODI YA MIKOPO MAONESHO YA TCU MNAZIMMOJA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 5 September 2020

WAZIRI MUSSA ZUNGU ATEMBELEA BANDA LA BODI YA MIKOPO MAONESHO YA TCU MNAZIMMOJA

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mussa Zungu (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mawasiliano Mkuu wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Veneranda Malima wakati alipotembelea Banda la HESLB jana Alhamisi (Septemba 3, 2020) katika Maonesho ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.



Maafisa wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) (kulia) Tuli Madhebehi na Saleko Mandara wakifafanua hoja na kujibu maswali kutoka kwa wateja mbalimbali waliotembelea Banda la HESLB jana Alhamisi (Septemba 3, 2020) katika Maonesho ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazimmoja Jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mussa Zungu (kushoto) akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea banda la Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Septemba 3, 2020 katika Maonesho ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Mawasiliano Mkuu wa HESLB, Veneranda Malima.


No comments:

Post a Comment