NAIBU Wiziri wa Kilimo Omary Mgumba amesema katika msimu ujao wa ununuzi wa korosho ghafi serikali imepanga kuweka utaratibu mahsusi wa viwanda vya kubangua korosho nchini kuwa na uahika wa malighafi.
Ametoa kauli hiyo mjini Mtwara wakati alipofungua kikao kazi cha kujadili mkakati huo wa kuviwezesha viwanda vya kunabgua korosho ndani ya nchi kupata malighafi ya kutosha huku ikihakikisha korosho ya wakulima inapata soko la uhakika.
“Tumekutana hapa kama serikali kujadili namna tutakavyowezesha viwanda vyetu 40 vya kubangua korosho ndani ya nchi vipate malighafi ya kutosha msimu huu 2020/2021,” alisema Mgumba.
Naibu Waziri huyuo alisema kuna viwanda 40 vya kubangua korosho nchini vyenye uwezo wa awali wa korossho tani 170,476 kwa mwaka lakini uwezo wa sasa ni kubangua korosho tani 59,776.
Naibu Waziri Mgumba alisema kikao hicho ni utekelezaji wa maagizo ya Rais John Pombe Magufuli kuhakikisha nchi inauza nje korosho ilioongezwa thamani ili kuwafanya wakulima wapate fedha nzuri na nchi ipate fedha za kigeni.
Lengo la uzalishaji korosho ghafi kufikia mwaka 2025 imepangwa kuongezeka toka tani 313,826 mwaka 2017/2018 hadi tani 1,000,000 ifikapo mwaka 2025 ambapo wizara ya Kilimo kupitia vituo vyake 17 vya utafiti wa kilimo (TARI) unaratibu upatikanaji wa mbegu bora za korosho.
Akiongea kwa niaba ya wakuu wa mikoa inayolima korosho nchini,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme alisema Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020 inasisistiza zao la korosho liongwezwe thamani hapa nchini ili lisaidie wakulima kupata uhakika wa soko na kuzalisha ajira kwenye viwanda.
Mndeme ameitaka pia wizara ya Kilimo kuweka mkazo katika utafiti wa mbegu bora za korosho na upatikanaji wa pembejeo kulingana na maeneo ya uzalishaji nchini ili uzalishaji uongezeke.
”Wizara ya Kilimo isimamie uapatikanaji wa mbegu mbegu bora na pembejeo za korosho zenye kutafitiwa kulingana na maeneo ya ikolojia ya uzalishaji nchini hali itakayokuza ualishaji na tija kwa mkulima“ alisema Mndeme.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa aliwaeleza wajumbe wa kikao hicho kuwa nchi inahitaji viwanda vingi vya kubangua korosho ili kuwahaikishia wakulima uhakika wa soko.
Alisema mkoa wa mtwara ndio unaoongoza kwa uzalishaji wakorosho nchini hali inayoufanya mkoa huo uwe na mazaingira mazuri ya kuwekeza viwanda.
“Wizara ya Kilimo pamoja na kuhamasisha ubanguaji wa korosho ifikirie kuongeza uzalsihaji wa korosho ghafi kwa wakulima wengi Zaidi kulima mashamba kwa kutumia mbegu bora na pembejeo za uhakika.
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya alisema wizara yake ipo katika mkakati wakufundisha maafisa ugani wa halmashauri zote zinazolima korsho ndani ya mikoa 17 kanuni bora za uzalishaji zao hilo ili kuongeza tija na kusaidia wakulima kuzalisha kwa ubora.
No comments:
Post a Comment