Na Prisca Ulomi, Chato
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt.Zainabu Chaula amezindua minara miwili ya mawasiliano iliyopo kwenye kijiiji cha Nyabilezi na Igando vilivyopo wilayani Chato mkoani Geita ili kuwawezesha wananchi kupata huduma za mawasiliano
Dkt. Chaula amesema kuwa ujenzi wa minara hiyo umefanyika kwenye vijiji hivyo baada ya wananchi kuomba huduma za mawasiliano na Serikali kujiridhisha kuwa mawasiliano hayapo kwenye maeneo hayo na kuamua kujenga minara hiyo kwa kutumia ruzuku ya Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) ambapo ujenzi wake umegharimu zaidi ya shilingi milioni mia tano
Ameongeza kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma za mawasiliano kwa kuwa mawasiliano ni uchumi na Serikali imefanya uwekezaji mkubwa kwa kujenga Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ambao ni sawa na barabara kuu kwa ajili ya kupitisha ya uhakika na kwa wakati ambapo minara hiyo imeunganishwa kwenye Mkongo huo ili kuweza kuwapatia wananchi huduma
Naye Katibu Tawala wa Mkoamwa Geita, Denis Bandesi amesema kuwa miundombinu ya mawasiliano ambayo imewekwa kwenye maeneo hayo itawasaidia wananchi kufanya mawasiliano na kuendesha biashara zao ili kuhakikisha kuwa uchumi wa kati unamgusa mwananchi pale alipo kwa maana uzalishaji atakaokuwa ameufanya atakuwa na uhakika wapi apeleke biashara yake kwa maana ya uhakika wa bei nzuri mahali soko lililopo.
Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhandisi Charles Kabeho, akizungumza na wananchi wa katika hafla ya uzindua mnara wa mawasiliano ya simu kijijini humo wilayani Chato, mkoani Geita. |
Wananchi wa Kijiji cha Igando wajitokeza kushiriki uzinduzi wa mnara wa mawasiliano katika hafla iliyofanyika katika Kijiji icho. |
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Waziri Kindamba amewataka wananchi kuchangamkia fursa ya kuwa mawakala wa huduma za mawasiliano wa Shirika hilo kwa kuwa TTCL inatoa kamisheni mara mbili ya kampuni nyingine za mawasiliano na fedha inayopatikana inarudi Serikalini na ameomba wananchi wailinde miundombinu hiyo kwa kuwa imetumia fedha za Serikali kujengwa na ikiharibika wananchi watakosa mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mhandisi Charles Kabeho ameahidi kuwa atahakikisha miundombinu hiyo inalindwa ili wananchi wanufaike na huduma za mawasiliano kwa kuwa hapo awali hapakuwa na huduma za mawasiliano ila kwa sasa mtandao wa TTCL uko vizuri na wananchi wanaweza kupiga simu ndani na nje ya Tanzania
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Justina Mashiba amesema kuwa UCSAF ina jukumu la kupeleka mawasiliano vijijini ambapo mpaka sasa UCSAF ina miradi ya ujenzi wa minara ya mawasiliano sehemu mbali mbali nchini kwenye kata 998 ambapo hadi sasa ujenzi umekamilika kwenye kata 903 ambapo zaidi ya wananchi wapatao milioni tano wanapata huduma za mawasiliano
No comments:
Post a Comment