WAZIRI
wa viwanda na biashara Innocent Bashungwa ameipongeza Benki ya NMB kwa utoaji
wa elimu ya kifedha bure kwa wajasiriamali mbalimbali kwenye maonesho ya Nane
Nane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Bashungwa
alisema kuwa jambo ambalo linalofanywa na benki hiyo kwenye maonesho hayo ni
muhimu sana hasa kwa wakulima, wavuvi na wafugaji ambao wana uhitaji mkubwa wa
elimu ya usimamizi wa fedha.
Waziri
huyo alisema hayo jana baada ya kutembelea banda la Benki hiyo wakati wa maonesho
hayo, ambapo alifurahishwa kukuta wakulima, wafugaji na wavuvi wamejitokeza kwa
wingi kupata elimu hiyo.
Alisema
kuwa lengo kubwa la serikali kuanzisha maonesho hayo ni kutaka wananchi walioko
kwenye sekta ya kilimo kuweza kupata teknolojia za kuwawezesha kuongeza tija
kwenye uzalishaji wao pamoja na mikopo.
“
Wamekuwa wakipata hizi teknolojia lakini bado tatizo lipo kwenye kujua wapi
wapate mikopo, lakini pia jinsi ya kusimamia pesa zao, nimefurahishwa sana
kuona hili NMB mnalitekeleza kwa ufanisi hapa Nanenane,” alisema Bashungwa.
Hata
hivyo Waziri huyo aliiomba benki hiyo kutoa elimu kama hiyo kwenye vyama vya
msingi vya ushirika (Amcos) ambavyo vimekuwa na matatizo ya ubadhilifu wa fedha
za wanachama.
“
Niwaombe NMB kuweza kuisadia serikali kutoa elimu hii kwa Amcos, baadhi yake
bado zina matatizo kwenye usimamizi wa fedha, ingawa serikali tumeendelea
kupambana nalo lakini elimu hii ni muhimu sana kwao,” alisema Bashungwa.
Kwa
upande wake Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Magharibi Sospeter Magesse, alisema
kuwa benki hiyo imeweza kutoa kiasi cha sh. Bilioni 161 kwenye mazao ya
Tumbaku, Kahawa na Pamba tangu mwanzoni mwa mwaka katika kanda hiyo.
Magesse
alisema kuwa kiasi hicho cha pesa kimepelekwa kwenye mazao hayo kama mkopo
ambapo wanufaika wakuu ni wakulima kupitia vyama vyao vya msingi (Amcos)
takribani 700.
No comments:
Post a Comment