NAIBU WAZIRI UJENZI AFURAHIA USHINDI WA TTCL NANENANE SIMIYU - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday 11 August 2020

NAIBU WAZIRI UJENZI AFURAHIA USHINDI WA TTCL NANENANE SIMIYU

Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias John Kwandikwa aliebeba kikombe pamoja na watumishi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) wakifurahia mara baada ya kuibuka washindi wa tatu  katika Maadhimisho ya Sikukuu ya wakulima, Nanenane yaliofanyika kitaifa mkoani Simiyu.

 

Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa  TTCL Corporation, Bw. Waziri Waziri Kindamba jana kikombe cha mshindi wa tatu wa jumla Maonesho ya Nanenane kitaifa yaliyofanyika kitaifa mkoani Simiyu Viwanja vya Nyakabindi.   

Wafanyakazi wa TTCL Corporation, pamoja na Mkurugenzi Mkuu wao Bw. Waziri Waziri Kindamba wakifurahiya kikombe cha mshindi wa tatu wa jumla Maonesho ya Nanenane kitaifa mkoani Simiyu Viwanja vya Nyakabindi.   


Mkuu wa Idara ya Mawasiliano Serikalini  Wizara ya Maliasili na Utalii, Bi. Dorina Makaya (wa pili kushoto) na Meneja Msaidizi Kanda ya Kati, Patricia Manonga ( wa tatu kulia), wakiwa na baadhi ya  watumishi wa wizara hiyo, Taasisi na vyuo wakisherehekea ushindi walioupata baada ya kukabidhiwa cheti cha ushindi wa kwanza katika kundi la sekta ya uchumi na uzalishaji wakati wa kilele cha Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Kati kwenye viwanja vya Nzuguni, jijini Dodoma.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia maswala ya Walemavu mhe. Stella Ikupa ( wa kwanza kulia) akimkabidi cheti kwa niaba ya Wizara ya Maliasili na Utalii  Mkuu wa Idara ya Mawasiliano Serikalini Bi. Dorina Makaya  (mwenye T-shirt nyeupe) na Bi. Patricia Manonga (wa kwanza kushoto) kwenye halfa ya kilele cha Maonesho ya Nane Nane  jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment