Mkurugenzi wa Uendeshaji wa maendeleo ya biashara UTT Amis Issa Wahichinenda akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kituo chao mapema leo jijini Arusha. |
Mkurugenzi wa masoko UTT AMIS Daud Mbaga akiongea na waandishi wa habari kwenye uzinduzi wa kituo cha Utt Amis kwenye Jengo la mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro jijini Arusha. |
Mwakilishi wa
benki ya CRDB Mery Mponda akiongea kwenye uzinduzi wa kituo cha
uwekezaji tawi la Arusha kwenye jengo la mamlaka ya hifadhi ya
Ngorongoro mapema leo jijini Arusha. |
UTT Amis imezindua rasmi kituo cha kuhudumia wawekezaji katika kutekeleza azma ya serikali ya awamu ya tano kufikia uchumi wa kati wa viwanda ambapo imetawaka wananchi mkoani hapa kuchangamkia fursa za
uwekezaji.
Akizungumza wakati akifungua kituo hicho katika jengo la mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro lililopo jijini Arusha Mkurugenzi wa Uendeshaji wa maendeleo ya biashara UTT Amis Issa Wahichinenda amesema kuwa msingi huo umepelekea mfuko huo kusogeza huduma karibu kwa wateja.
Alisema kuwa mfuko huo wa utt Amis ni kampuni ya serikali yenye lengo la uendeshaji wa mifuko 6 ya uwekezaji wa pamoja na kuwa wanatoa huduma za usimamizi wa mitaji binafsi yote ikitekelezwa kwa sheria ya masoko na mitaji ya dhamana ya mwaka 1994 na marekebisho yake na kanuni za mifuko ya uwekezaji wa pamoja ya mwaka 1997.
Alieleza kuwa kuweka katika mifuko ya uwekezaji wawekezaji wananufaika na unafuu wa gharama za uwekezaji utaalam wa uendeshaji kupitia meneja wa mfuko pia wawekezaji wanauwezo wa kufuatilia uwekezaji wao na kujua hali ua uwekezaji wao na soko kwa ujumla.
Alisema kuwa mifuko hiyo imeandaliwa mahsusi kwa wawekezaji wadogo kama vile mamalishe madereva bodaboda wachuuzi wadogo na wakubwa huku ukuzingatia malengo yao ya uwekezaji muda wa kuwekeza ukwasi uwezo wa kuhimili changamoto za uwekezaji na usalama.
“Mathalan mfuko wa umoja kiwango cha kuanzia kuwekeza ni vipande 10 tu sawa na wastani wa takribani tsh.6500 huku mfuko wa uwekezaji maisha unatoa faida pacha za uwekezaji ikiendana na bima ya maisha ya kiwango cha chini tsh.8340 iwapo mwekezaji atachagua mpango wa kuwekeza kila mwezi.
Awali mkurugenzi wa masoko wa UTT AMIS Daud Mbaga alisema kuwa msingi wa mkuu wa wakazi wa mkoa wa Arusha ni kuchukuwa fursa hiyo kuwekeza nao kwa kuendana na dhana ya serikali kufikia uchumi wa kati wa
viwanda.
Alisema kuwa kuanzishwa kwa mfuko huo wa uwekezaji wa pamoja yalikuwa ni maksudi ya serikali kwa mwananchi wa chini kabisa kuwekeza fedha zake kwa senti ndogo na kuendelea kukuza kipato chake kwa kuwekeza.
Nae Meneja wa CRDB alisema kuwa ushirikiano wao na mfuko huo wa uwekezaji utasaidia kuongeza tija za kiuchumi kwa wananchi wa hali ya chini ambao wanahitaji kukuza mitaji yao kufikia malengo yao ya
kiuchumi.
Alisema kuwa wamekuwa wakishirikiana na mfuko huo bega kwa bega katika zaidi ya matawi yao 10 yaliopo katika jiji la Arusha na mawakala wao hivyo ufunguzi wa ofisi hizo utasaidia kuongeza tija kwa wananchi na kusogeza huduma kwa umoja wao.
“Niwaombe wakazi wa mkoa wa Arusha kuitikia suala zima la uwekezaji wa mfuko wa UTT amis kwa lengo la kuisaidia serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi wake hivyo fursa hiyo sio ya kuicha iwapite hivi
hivi,”alisema.
No comments:
Post a Comment