Barabara za kisasa zinazoendelea kubadili taswira za nchi ya Tanzania. |
Na David KAFULILA
JULAI MOSI, 2020 ni tarehe itakayobaki kwenye kumbukumbu kama siku ya kwanza ya kuanza kwa utekelezaji wa Bajeti ya tano na ya mwisho ya kumalizia miaka5 ya kwanza ya awamu ya tano.
Siku ambayo Benki ya dunia ilitambua Tanzania kuwa nchi ya Uchumi wa kati, ikiwa ni miaka5 kabla ya kufikia mwaka 2025. Katika kujadili mafanikio haya ningependa kukumbusha rekodi SABA (7) za JPM kimataifa kama sehemu tu kutafsiri mafanikio haya kwa kumbukumbu za kizazi hiki na kijacho;
# Kwanza, nikuweka kumbukumbu kwamba wote waliokuwa wakijiuliza JPM ANAJENGA nchi ya namna au analipeleka wapi Taifa hili kama ilivyo kwenye topic moja jukwaa maarufu la jamiiforum,
Julai mosi, 2020 ,Benki ya dunia wamejibu!
Wamejibu kwamba JPM alikuwa anatuleta uchumi wa kati kabla ya mwaka 2025!
# Pili, rekodi iliyotolewa na IMF kupitia aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika hilo, Bi Christine Legarde alipohojiwa na Jarida maarufu la Quartz, mwaka 2017 akiwa Addis nchini Ethiopia,
Alipoulizwa ni nchi zipi Afrika zinaelekea Vietnam kwa mapinduzi ya viwanda, alizitaja Tanzania , Ethiopia , Nigeria na Kenya. Hili ilikuwa jibu kwa watanzania waliokuwa wakihoji kama kweli Serikali ya JPM inajenga uchumi wa viwanda.
Kwamba kinachoendelea Tanzania kuhusu ujenzi wa viwanda kinatambulika duniani!
# Rekodi ya tatu ni ile iliyotolewa kwenye jukwaa la kimataifa kuhusu Uchumi ( World Economic Forum 2018), ambapo Tanzania ilitajwa kuwa Taifa kinara Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara kwa uchumi jumuifu kwa maana ya uchumi unaobeba watu wengi ( inclusive economy).
Rekodi hii ilikuwa inajibu kama kweli Serikali ya awamu ya 5 ni Serikali ya wanyonge kweli au la!
# Rekodi ya nne, ni Serikali ya Tanzania kutajwa kuwa ya 28 kati ya nchi 186 duniani zilizofanyiwa tathimini kwa umadhubuti katika usimamizi wa matumizi fedha za umma.
Baadhi ya nchi zilizochwa mbali na nafasi zao kwenye mabano ni Kenya(70), Uganda(100), Malawi (106), Msumbiji (118), Ghana(61), Botswana (37).
Rekodi hii inathibitisha kuwa hata dunia inatambua kuwa JPM ANAJENGA Serikali yenye nidhamu ya matumizi hata kuwa na rekodi kubwa sio tu Afrika bali duniani. Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya World Economic Forum, Excutive Opinion Survey 2019).
# Rekodi ya tano, ni Tanzania kutajwa kama Taifa kinara katika nchi 37 Afrika zilizofanyiwa utafiti katika vita dhidi ya ufisadi. Hii ni kwa mujibu wa Ripoti ya The Africa global opinion survey 2019.
Tumetoka mbali jamani! mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni!
zama za kukodi ndege mbovu kwa dola milioni 43, inafanya kazi miezi 6 lakn miezi37 ipo gereji ilikuwa mateso kwa Taifa hili la Mungu...( rejea ripoti ya CAG Aprili2020).
leo chini ya JPM Serikali inanunua ndege mpya bombardier kwa dola milioni32, kiasi ambacho ni chini ya tulichotumia kukodi ndege mbovu iliyoishi gereji robo tatu ya muda wa mkataba,
Huu ni mfano mdogo tu kuonesha kwamba kama Taifa kuna miongo kadhaa tulipoteza na sasa Taifa linachukua heshima na nafasi yake !
# Rekodi ya sita ni imani ya wananchi kuwa Serikali yao inapambana na ufisadi, ambapo asilimia 72 ya watanzania walijibu kuwa Serikali ya Tanzania kweli inapambana na ufisadi ukilinganisha na asilimia 13 mwaka 2015( ripoti ya Africa Global opinion survey 2019).
Hii ni moja ya rekodi ya mapinduzi makubwa sana duniani. Kuna mtaalamu mmoja alinichekesha kusema kwamba kuruhusu ufisadi pengine ilikuwa 'Expansionary policy'! Kwamba ufisadi uliruhusiwa kutanua matumizi kujenga uchumi!
Kwakweli uchumi unajengwa kwa mtindo huo ilikuwa uchumi wa' mishenitauni'..
# Rekodi ya Saba ni Tanzania kufanyiwa tathimini ya kimataifa kuhusu umadhubuti wa kiuchumi na kiubuka kinara Afrika mashariki kiasi cha kuzua taharuki nchini Kenya ( rejea Gazeti la nchini Kenya - The BusinessDaily, March4,2017).
Hii ni kwa mujibu wa tathimini ya Taasisi ya Kimataifa- The Moodys yenye makao makuu nchini Marekani.
Taasisi hiyo ambayo inaongoza duniani kwa kufanya tathimini hizi( Credit rating) ilifanya tathimini hii ya kwanza kufanywa Tanzania tangu tupate uhuru na ikaipa Tanzania daraja la B1 ikiwa juu ya nchi zote za Afrika mashariki zenye daraja B2.
Hizi nikumbukumbu za dunia na zitabaki hivyo kama utambulisho wa JPM kimataifa achilia mbali kumbukumbu ya diplomasia kubwa aliyoitumia kukabili ugonjwa wa corona na kuziacha nchi zote duniani zikijiuliza iliwezekanaje corona iliyoyumbisha dunia nzima lakn ikashindwa Tanzania ya JPM.
Ninachosisitiza hapa nikwamba wakati JPM akifanikisha rekodi kubwa kiasi hiki kitaifa na kimataifa, vema tukakumbuka kuwa alipokea Serikali mwaka 2015 ikiwa hoi kiasi haikuwa na uwezo wa kulipa mshahara na deni la Taifa kwa mwezi.
Alipokea Serikali ambayo ililazimu kukopa ili kulipa mshahara na hivyo kukopa soko la ndani kwa riba kubwa ya asilimia 17 kwa hati fungani za mwaka mmoja kulinganisha na sasa ambapo Serikali inakopa kwa riba ya asilimia 4.8.
Serikali yenye dhiki inakopa kwa riba yeyote ( desperate government)!.... Ndani ya miaka5 JPM amefanikisha rekodi kubwa nchini kwenye kila sekta inayohusu maendeleo ya watu!.
Amefanikisha kujenga Serikali yenye msuli kiuchumi katika tafsiri zote kiuchumi nchini na duniani.
Tuliojua rekodi hizi hatukushangaa kusikia rekodi ya Bank ya dunia kwa Tanzania kutangazwa kufuzu kuingia uchumi wa kati miaka 5 kabla ya mwaka wa lengo ambao 2025.
No comments:
Post a Comment