TAFSIRI YA TANZANIA KUINGIA KWENYE UCHUMI WA KATI... - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 2 July 2020

TAFSIRI YA TANZANIA KUINGIA KWENYE UCHUMI WA KATI...

Reli ya kisasa inayoendelea kujengwa nchini Tanzania

Ndugu zangu,

Zimetufikia leo Julai Mosi habari njema, kuwa Benki ya Dunia imeitangaza Tanzania kuwa Nchi ya Uchumi wa Kati.

Nini Tafsiri yake?

Nchi inapowekwa kwenye daraja hilo la kiuchumi kuna faida kadhaa kwa nchi husika;

- Hutoa tafsiri ya kuaminika kimikopo. Kwamba nchi inakopesheka. Tanzania chini ya Dr. John Magufulo imekuwa ikikopa kimikakati. Ni mikopo ya kujenga na kukarabati miundo mbinu ikiwamo reli, barabara na madaraja. Ni kwenye elimu na afya pia.

- Kwamba ina uhimili wa kiuchumi- stable micro-economy.
- Ina sera nzuri za kiuchumi zenye kuweka mazingira mazuri ya kuvutia wawekezaji. Ni wawekazaji wa ndani na uwekezaji wa moja kwa moja wa kutoka nje kwa maana ya Foreign Direct Investment.

Hilo la mwisho huleta tija zaidi ya hata misaada ambayo nchi hupokea. Hapa kukiwa na mikataba yenye maslahi ya uwekezaji nchi huvuna zaidi.

Ni hapa pia uongozi wa Rais Dr. John Magufuli unastahili pongezi kwa kukomaa na wawekezaji kwenye mikataba ya uwekezaji sekta ya madini. Mikataba ambayo imelinda maslahi ya nchi.

Je, Uchumi wa Kati ina maana ya raia kujazwa mapesa mifukoni?

Jibu:
La hasha, uchumi wa kati haina maana ghafla maisha ya watu kwa maana ya vipato vyao vitabadilika na kuongezeka.

Umasikini wa vipato kwa wengi utabaki, isipokuwa, usimamizi mzuri wa mapato ya Serikali na uendelelezaji wa miundo mbinu utatoa fursa zaidi kwa raia kujipatia vipato zaidi. Ni kwa kufanya kazi kwa bidii.

Maggid Mjengwa.

Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment