MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM RAIS DKT. MAGUFULI AWAALIKA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CCM IKULU YA CHAMWINO MKOANI DODOMA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 13 July 2020

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM RAIS DKT. MAGUFULI AWAALIKA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CCM IKULU YA CHAMWINO MKOANI DODOMA

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma kwa ajili ya hafla ya chakula cha mchana aliowaandalia Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM tarehe 12 Julai 2020.

Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM pamoja na viongozi wengine wakiweka zege kama kumbukumbu katika ujenzi wa Ofisi mpya za Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. 

Baadhi ya Mawaziri wakicheza nyimbo zilizokuwa zikitumbuizwa katika hafla maalumu ya Chakula cha Mchana iliyoandaliwa na Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akicheza mziki uliokuwa ukipigwa na Msanii Hamza Kalala na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally Kakurwa katika hafla hiyo ya Chakula cha Mchana kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu.

Viongozi Wastaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM pamoja na Wajumbe wengine wa Mkutano Mkuu wakicheza mziki katika hafla ya Chakula cha Mchana kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM iliyoandaliwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Msanii wa Kizazi kipya Ali Kiba akitoa burudani katika hafla hiyo ya Chakula cha Mchana katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Msanii wa Kizazi kipya Ali Kiba akitoa burudani katika hafla hiyo ya Chakula cha Mchana katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino kwa ajili ya hafla ya chakula cha mchana iliyowandalia Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM. PICHA NA IKULU.

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwasili katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino kwa ajili ya hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Mwenyekiti wa CCM Rais Mhe. Dkt. Magufuli kwa ajili ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM.


No comments:

Post a Comment