MAGARI YA DHARULA NI YAPI, NA JE YANARUHUSIWA KUVUNJA SHERIA? - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 2 June 2020

MAGARI YA DHARULA NI YAPI, NA JE YANARUHUSIWA KUVUNJA SHERIA?


MAGARI YA DHARULA NI YAPI, NA JE YANARUHUSIWA KUVUNJA SHERIA?

[Kifungu cha 54 cha Sheria ya Usalama Barabarani]

1. Bila kujali vifungu vya sheria ya Usalama Barabarani na kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 54, dereva wa gari la dharula, ikiwa ataona kuwa kuzingatia sheria kutazuia matumizi ya gari la dharura kwa kusudia lililotarajiwa, anaweza kufanya lolote kati ya yafuatayo:

(a) Kuegesha gari mahali popote barabarani bila kujali sehemu hiyo ni maegesho au la

(b) baada ya kupunguza mwendo kadiri itakavyokuwa salama, akaipita alama inayomlazimu kusimama

(c) kuzidisha mwendo kupita ule unaoruhusiwa kwenye barabara hiyo ili mradi tu hahatarishi maisha au mali; au

(d) anaweza kupuuza sheria yoyote inayoongoza muelekeo wa magari au kupinda kwenye muelekeo wowote.

Masharti ya kifungu hiki.

2. Ruhusa iliyotolewa na kifungu hiki kwa magari ya dharula itatumika tu pale ambapo dereva wa gari hilo awapo kwenye mwendo atakuwa anapiga kingóra au filimbi, kadiri inavyowezekana au pale ambapo gari litakuwa na kimulimuli basi atawasha kimulimuli kitakachoonekana wakati wote kwa umbali wa mita 150 toka mbele ya gari.

3. Masharti ya kifungu hiki hayatamuondolea dereva wa gari la dharula wajibu wa kuchukua tahadhari  na kuendesha kwa umakini kwaajili ya usalama wa watu au mali, na hakitamlinda dereva kutokana na madhara ya kutoendesha kwa umakini (uzembe) utakaosababisha madhara kwa watu au mali.

4. Kwa minajili ya kifungu hiki magari ya dharula inamaanisha magari ambayo yanatumika mara kwa mara kwa shughuli za polisi, zimamoto, magari ya wagonjwa, magari ya majeshi, na magari mengine ambayo kwa amri ya Waziri iliyochapishwa kwenye gazeti la serikali yatatajwa kuwa ni ya dharula.

Admin 1

RSA Tanzania
Usalama barabarani ni jukumu letu sote

No comments:

Post a Comment