Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Fortunatus Muslim, akizungumza na madereva wa malori eneo la Mizani Mjini hapa wakati wa ziara yake ya siku moja ya kikazi aliyoifanya jana.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Fortunatus Muslim, akizungumza na Askari wa Usalama Barabarani Mkoa wa Singida katika eneo la Mizani.
Mazungumzo na askari hao yakiendelea.
Kamanda Muslim akisisitiza jambo.
Kamanda Muslim akizungumza na madereva.
Na Dotto Mwaibale, Singida
KAMANDA wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini,
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Fortunatus Muslim ametoa elimu ya
kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa
Covid 19 kwa watendaji wa jeshi hilo, madereva na abiria mkoani Singida.
Akizunguza na waandishi wa habari mjini hapa jana
alisema amefika kwa ziara ya siku moja ya
kwa ajili ya ukaguzi wa kawaida wa barabarani na kuangalia hali ya
utendaji wa askari wa jeshi hilo na mwenendo wa vyombo vya moto.
Alisema nia kubwa ni kutoa elimu na kuhakikisha
kwamba wanathibiti ajali za barabarani na kukumbushana kuchukua tahadhari ya
ugonjwa wa Corona.
" Leo nimeanza kufanya kazi eneo la
Mizani pale Njuki kwa kuzungumza na
madereva wa malori kuhusiana na mwendo kwamba bado ni tatizo na kuwa ni chanzo
kikubwa cha ajali zinazotokea barabarani
nimetoa mfano wa ajali iliyotokea mkoani Mwanza ambapo lori lilikwenda kugonga
trekta ambalo lilipoteza mwelekeo na kwenda kugonga gari la abiria na
kusababisha vifo vya watu nane huku watano wakijeruhiwa" alisema Kamanda
Muslim.
Alisema alikuwa anajaribu kuonesha madhara yanayosababishwa na mwendo kasi kwamba tumepoteza watanzania ambao tulikuwa
bado tunawahitaji kwa kufanya kazi ili kuweza kuinua uchumi na kuleta maendeleo
ya nchi yetu.
Muslim alisema pia ametoa elimu kwa madereva kuhusu matumizi ya tochi wanazozitumia kukamata mwendo wengi wamekuwa
wakilalamika kwamba picha zinazopigwa na kutumwa kwenye simu zinachezewa wakati
sio kweli hivyo nimewaonesha namna gani tochi hizo zinavyounganishwa kwenye
simu na kwamba muungano huo unafanyika ndani kwa ndani ya
ile kamera na askari hawezi kuifanyia mabadiliko yoyote.
Alisema hivi sasa wapo kwenye utaratibu wa kuanza
kutumia kifaa kipya ambacho watakitumia kupokea hizo picha kwa nchi nzima hivyo amewasihi wazingatie sheria, alama na michoro ya barabarani badala ya
kuendesha huku wakitafuta askari yupo wapi.
Muslim alisema amewaambia madereva hao kuyaondoa
magari yao barabarani pale yanapokuwa yameharibika kwa kuyatengeneza haraka na
waache tabia ya kuweka majani na miti kwani inapofika usiku magari mengine
yakijaribu kuyapita wanashindwa kuyaona hivyo kujikuta wakiyagonga na
kusababisha ajali.
Akitolea mfano alisema juzi waliyakamata mabasi
mawili yaliyokuwa yakipishana mlima Saranda ambapo alizungumza na madereva wa
malori kuwa kuanzia sasa hawatasimamishwa katika sehemu nyingine yoyote
isipokuwa kwenye maeneo ya mizani.
Alisema sehemu nyingine wanazoweza kusimamishwa ni iwapo kutakuwa na taarifa za kiinterejesia kwamba yamebeba vitu kinyume cha
sheria au yamesababisha ajali au yamefanya makosa barabarani au kama madereva
hao leseni zao zinadaiwa faini za makosa ya usalama barabarani hivyo amewataka
walipe ili kuepuka kusimamishwa hovyo barabarani kwa ajili ya hayo madeni.
Alisema akiwa Stendi Kuu ya Mabasi Mkoa wa
Singida amezungumza na madereva na kuwasisitizia kuacha kwenda mwendo wa kasi
kwani Serikali yetu ni sikivu imeruhusu kusafiri usiku hivyo hakuna sababu ya
kwenda kwa mwendo wa kasi.
No comments:
Post a Comment