Rais wa Chama cha Madaktari nchini Tanzania (MAT) Dkt Elisha Osati. |
Katika mahojiano maalumu na BBC, Osati amekanusha kuwa mfumo wa afya nchini humo umeelemewa na wagonjwa. Ameeleza pia wengi wa wagonjwa wa corona nchini humo walikuwa na dalili za kati.
Hii ni mara ya kwanza kwa mwanataaluma ya afya nchini Tanzania kutoa tathimini kuhusu ugonjwa huo nchini humo. Maelezo hayo ya Osati hata hivyo yanapishana na baadhi ya watu nchini humo ambao wanatahadharisha kuwa hali ya ugonjwa huo inaweza kuwa mbaya.
Wiki mbili zilizopita, Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ulitoa tahadhari kuwa hospitali jijini Dar es salaam zimeelemewa kwa wagonjwa, lakini hawakutoa ushahidi wa madai hayo.
Rais John Magufuli pamoja na viongozi wengine waandamizi wanasisitiza kuwa idadi ya wagonjwa imeshuka, hali iliyosababisha kuruhusu ndege za kimataifa za abiria, kufunguliwa kwa vyuo vikuu, kidato cha sita na michezo ya ligi kuu.
-BBC
No comments:
Post a Comment