RAIS MAGUFULI AFUNGUA RASMI VYUO NA MICHEZO TANZANIA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday 21 May 2020

RAIS MAGUFULI AFUNGUA RASMI VYUO NA MICHEZO TANZANIA

Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi mbalimbali aliowaapisha leo tarehe 21 Mei 2020 katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo mara baada ya kuzungumza na viongozi mbalimbali aliowaapisha katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. PICHA NA IKULU.

Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi mbalimbali aliowaapisha leo tarehe 21 Mei 2020 katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli leo amevifungua vyuo vyote nchini, pamoja na michezo baada ya kujiridhisha kupungua kwa maambukizi ya ugonjwa wa Corona unaosumbua mataifa mengi ulimwenguni kwa sasa. Amesema wanafunzi wote wanatakiwa kwanza masomo Juni Mosi, 2020.

Akinzungumza leo katika Ikulu ya Chamwino alipokuwa akiwaapisha viongozi wateule, Rais Magufuli amesema Serikali inafuatilia mwenendo wa hali kabla ya kuzifungua pia shule za msingi na Sekondari.

Amesema agizo la leo linakwenda sambamba na kuifungua michezo yote nchini iliyokuwa imesimama baada ya kuingia ugonjwa wa Corona nchini ikiwa ni mikakati ya kukabiliana nao ili usisambae zaidi.

Aidha ameelekeza wanafunzi wa kidato cha sita waliokuwa wakitarajia kuanza mitihani yao nao kurejea Juni Mosi, 2020 na Wizara ya Elimu kuanza kuwaandaa kabla ya kuanza mitihani yao ya mwisho.

Sambamba na hilo Rais ametangaza ndege za watalii waliokuwa wameomba kutembelea Tanzania kuanza kutua nchini Mei 27 na 28, 2o2o ili kuendelea na ratiba zao za kitalii. Ameshauri wananchi kujitokeza kuomba kwa imani zao kuanzia siku ya Ijumaa, Jumamosi na Jumapili kumshukuru Mungu kutenda miujiza kipindi hiki cha ugonjwa wa virusi vya covid19 kuiepusha nchi kuingia kwa maambukizi makubwa.

Hata hivyo amewataka kuendelea kuchukua tahadhari kwani bado ugonjwa haujaondoka kabisa Tanzania.

No comments:

Post a Comment