Pichani Sheikh na Kadhi wa mkoa wa Arusha Shaaban bin Jumaa akiongea akiwa na viongozi wa dini mkoani hapa picha na Ahmed Mahmoud Arusha |
WAISLAM nchini wameaswa kufuata miongozo ya mazishi yao sanjari na taratibu za Serikali kipindi chote cha Majanga ya magonjwa ya milipuko ikiwemo Ugonjwa wa homa kali ya mapafu Covid 19.
Kauli hiyo imetolewa na Sheikh wa mkoa wa Arusha Shaaban Jumaa mara baada ya Swala ya Ijumaa iliyofanyika kwenye Msikiti mkuu wa Ijumaa jijini Arusha wakati akiongea na vyombo vya habari mkoani hapa.
Alisema kuwa uislamu haukuacha kitu umeeleza kila jambo ikiwemo suala zima la kuwekwa Karantini kutokana na majanga ya magonjwa ya milipuko ukiwemo huu wa sasa Covid 19 pamoja na kuwazika maiti wao.
"Uislamu kupitia kwa Mtume Muhammad S.A.W umeweka utaratibu wa maziko ya waislamu na juu ya kuwakinga waislam kupata maradhi hayo hivyo lazima tununue sanda na vifaa vya kuoshea maiti zetu ili kuwakinga wenzetu"
Kwa mujibu wa Sheikh Shaaban kwetu sisi hapa nchini maiti zetu tutafuata utaratibu tuliokubaliana na viongozi wa Idara za Afya chini ya timu yao inayoshughulikia suala hili ila kila muislamu atalazimika kununua nguo maalumu za kuoshea maiti kama anavyofanya kununua sanda.
Aidha ameeleza kuwa Swala ya Idd el Fitry itaswalia edha siku ya Jumapili au Jumatatu kutokana na muandamo wa mwezi kama ilivyo mafundisho ya Uislamu fungeni kwa kuuona na fungeni kwa kuuona ndio msimamo wa baraza kuu kupitia baraza la Ulamaa hivyo waislam tuvaae barakoa tutakapokuja kuswali Swala ya Idd.
Kwa Upande wake Katibu wa bakwata mkoa wa Arusha Ally Othman Nassoro alisema baraza hilo litaendelea kushirikiana na Serikali katika kuondoa changamoto zao ndio maana kwa sasa unaona utaratibu huu.
Alisema kuwa Magonjwa ya milipuko ikiwemo homa kali ya mapafu Covid 19, kipindupindu au Ebola kama bakwata tutaendelea kufuata utaratibu tuliokubaliana na serikali kuzika maiti zetu kwa utaratibu wa kiislamu ili kitunza heshima na utu sanjari na kuwakinga wale watakao mshughulikia maiti mwenye kadhia hizo.
Alisema wameendelea kushirikiana na idara za afya sanjari na kuendelea kuwatoa hofu watanzania ikiwemo kutoa elimu ya Ugonjwa wa homa kali ya mapafu Covid 19 ili kuona Ugonjwa huo unaondokwa kwenye jamii zetu.
Nae Mmoja wa wajumbe wa Baraza hilo Ferooz Khan alisema bei ya vazi la kuoshea maiti wa Ugonjwa wa Covid 19 linauzwa kwa tshs.32,000 sambamba litauzwa na Sanda kwa maiti ambazo zitagundulika zina Ugonjwa huo ambao hapa nchini kwa mujibu wa Rais Magufuli idadi imepungua.
"Utaratibu huu wa kuzika maiti zetu kwa kutumia vazi maalumu la kuoshea unafanyika wakati huu nchi ikipitia kwenye janga la Covid 19 na hii ni kwa mujibu wa mafundisho ya Dini yetu kama alivyoelekeza bwana mtume S.A.W.
No comments:
Post a Comment