ILEMELA KINARA ZOEZI LA URASIMISHAJI MAKAZI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday, 5 April 2020

ILEMELA KINARA ZOEZI LA URASIMISHAJI MAKAZI

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimkabidhi Hati ya umiliki ardhi Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega wakati wa zoezi la ugawaji hati katika Manispaa ya Ilemela mkoa wa Mwanza jana.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza wakati wa zoezi la ugawaji hati miliki za ardhi kwa wananchi wa Manispaa ya Ilemela mkoa wa Mwanza jana. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela ambaye ni Afisa Ardhi na Mipango wa Manispaa hiyo Shukran Kyando na wa pili kushoto ni Afisa Ardhi mkoa wa Mwanza Elia Kamyanda

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela ambaye ni Afisa Ardhi na Mipango wa Manispaa hiyo Shukran Kyando akizungumza wakati wa zoezi la utoaji hati miliki kwa wananchi wa Ilemela jana. Kulia ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula na katikati ni Afisa Ardhi mkoa wa Mwanza Elia Kamyanda

Na Munir Shemweta WANMM, ILEMELA

HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilemela mkoa wa Mwanza imeendelea kuongoza katika zoezi la urasimishaji na umilikishaji makazi holela nchini kwa kuandaa michoro ya mipango miji 58,000, kupima viwanja 52,000 na kumilikisha jumla ya viwanja 72,000.

Hayo yalibainika jana katika viwanja vya Manispaa ya Ilemela mkoani Mawanza wakati wa zoezi la ugawaji hati miliki za viwanja 1,508 kwa wananchi wa wilaya ya Ilemela lililofanywa na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angelene Mabaula.

Dkt Mabula ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela alisema, ameridhishwa na kasi ya upimaji na umilikishwaji ardhi unaofanywa na wataalamu wa wilaya ya Ilemela sanjari na kuwaasa wananchi waliokabidhiwa hati zao kumshukuru na kumpongeza Rais John Pombe Magufuli kwa kuridhia kufanyika zoezi hilo.

‘’Pamaoja na changamoto zote mlizonazo, bado wilaya yetu ya Ilemela inaoongoza katika zoezi la urasimishaji, hongereni sana na hata mhe Waziri wa Ardhi amekuwa akiwapongeza mara kwa mara’’ alisema Dkt Mabula

Kupitia zoezi hilo Naibu Waziri wa Ardhi ameendelea kuzikumbusha kampuni za upimaji zinazoendesha zoezi la urasimishaji makazi kutekeleza agizo la Waziri wa Ardhi William Lukuvi la kukamilisha kazi zote zilizobaki ili kwenda  sambamba na kasi ya serikali ya awamu ya tano na kuwaondelea adha wananchi wanaohitaji huduma hiyo.

Kwa upande wake Afisa Mipango Miji wa mkoa wa Mwanza Deogratias Kalemenze alisema katika kipindi cha miaka ya 1990 mtu yeyote aliyejenga bila kufuata sheria na taratibu alilazimika kubomoa na kujenga upya tofauti na ilivyo sasa ambapo analazimika kulipia gharama kidogo na kumilikishwa na kusisitiza wananchi kuitumia fursa ya urasimishaji kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ambaye pia ni Afisa Ardhi na Mipango Miji wa Manispaa hiyo Shukran Kyando alielezea changamoto kubwa inayolikabili  zoezi la urasimishaji makazi katika manispaa yake kuwa ni kasi ndogo ya wananchi kulipia gharama za urasimishaji. Hata hivyo, alibainisha kuwa halmashauri ya Ilemela katika jitihada za kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa imeamua kutoa ilani ya siku 30 ya kuwataka wananchi hao kwenda kumilikishwa ardhi yao.

Mmmoja wa wananchi aliyekabidhiwa hati Veronica Byengo kutoka mtaa wa Ghana alimshukuru Rais JohPombe n Magufuli kwa uamuzi wake wa kuruhusu zoezi la urasimishaji makazi holela na kuwaomba wananchi wenzake kujitokeza kumilikishwa ardhi ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima na kuweza kukopesheka katika taasisi za fedha.

No comments:

Post a Comment