Wajumbe wa baraza la chuo wakikagua majengo ya Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam-Tegeta.
Wajumbe wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe wakimsikiliza Mwenyekiti wa baraza hilo, Prof.
Matthew Luhanga (wa pili kushoto), wakati walipofanya ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya ukarabati na ujenzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam-Tegeta jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe wakiingia katika moja ya majengo wakati walipofanya ziara ya ukaguzi
wa maendeleo ya ukarabati na ujenzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar
es Salaam-Tegeta jijini Dar es Salaam.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka, akifafanua jambo mbele ya wajumbe wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe, walipofanya ziara ya ukaguzi
wa maendeleo ya ukarabati na ujenzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar
es Salaam-Tegeta jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe wakimsikiliza Mwenyekiti wa baraza hilo, Prof.
Matthew Luhanga (wa pili kushoto), wakati walipofanya ziara ya ukaguzi
wa maendeleo ya ukarabati na ujenzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar
es Salaam-Tegeta jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Prof. Honest Ngowi (katikati), akizungumza na wajumbe wa baraza la chuo hicho.
Mwakilishi wa Mjumbe wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe, Julius Masota ambaye ni Ofisa Mkuu Msimamizi wa Fedha kutoka Wizara ya Fedha na Mipango akifafanua jambo wakati wa ziara hiyo.
Mwakilishi wa Mjumbe wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe, Julius Masota ambaye ni Ofisa Mkuu Msimamizi wa Fedha kutoka Wizara ya Fedha na Mipango akifafanua jambo wakati wa ziara hiyo.
Picha ya pamoja.
Na Mwandishi Wetu
MWENYEKITI wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Matthew Luhanga, ameongoza ujumbe wa baraza hilo kukagua maendeleo ya ukarabati na ujenzi wa miundombinu na madarasa kwa ajili ya kuanzisha Shahada za Awali Kampasi ya Dar ss Salaam.
Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka, amesema ukarabati huo na ujenzi umekamilika kwa asilimia 98, na kwamba majengo hayo yako tayari kutumika pindi idhini ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania itakapotolewa.
Baraza limepongeza hatua hiyo na kupendekeza ujenzi unaoendelea kuendana na mahitaji ya sasa ya mabadiliko ya teknolojia, kwa kuwezesha matumizi ya teknolojia katika ufundishaji.
No comments:
Post a Comment