MKATABA MPYA WA USHIRIKIANO KATI YA TANZANIA NA EU UIMARISHE SEKTA ZA MAENDELEO - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 24 February 2020

MKATABA MPYA WA USHIRIKIANO KATI YA TANZANIA NA EU UIMARISHE SEKTA ZA MAENDELEO

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akipeana mkono na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Mhe. Manfredo Fanti, baada ya kumaliza kwa mkutano kuhusu ushirikiano wa maendeleo ya kiuchumi, uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango,  jijini Dodoma.

Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Mhe. Manfredo Fanti, akizungumza kuhusu uboreshaji wa miundombinu ili kuchochea biashara, wakati wa kikao na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani), jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Adolf Ndunguru (kushoto) akizungumza jambo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) wakati wa kikao na Balozi wa Umoja wa Ulaya Mhe. Manfredo Fanti (hayupo pichani), jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akieleza umuhimu wa kuendeleza miradi ya maendeleo ambayo tayari inatekelezwa katika mkataba mpya wa Ushirikiano na Umoja wa Ulaya (EU) wakati wa mkutano na Balozi wa EU nchini, Mhe. Manfredo Fanti, jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akifafanua jambo kwa Waziri wa Ushirikiano wa Biashara wa Finland, Mhe. Ville Skinnari (kushoto), wakati wa wakati wa mkutano uliofanyika, jijini Dodoma.


SERIKALI imeuomba Umoja wa Ulaya (EU) kuwekeza katika maeneo ya maendeleo ambayo tayari Serikali imeanza kuyatekeleza ikiwemo uboreshaji wa miundombinu katika mkataba mpya wa ushirikiano kati ya Tanzania na EU kwa mwaka 2021 hadi 2027.

Hayo yameelezwa jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Tanzania, Mhe. Manfredo Fanti, kuhusu ushirikiano wa maendeleo ya kiuchumi.

Dkt. Mpango alisema kuwa, katika mkataba mpya wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na EU unaotarajiwa kuanza kutekelezwa mwaka 2021 ni vema ukaendelea kuimarisha maeneo ya maendeleo ambayo tayari yameanza kutekelezwa na Serikali hususani katika Sekta ya Elimu, Afya, miundombinu na mingine ili kufikia malengo endelevu.

Kwa upande wake Balozi wa EU nchini Tanzania, Mhe. Manfredo Fanti, aliipongeza Serikali kwa kuwa na Sera nzuri za maendeleo lakini pia akasema kuwa ili kuboresha mazingira ya kibiashara, miongoni mwa mambo yanayohitajika ni pamoja na Miundombinu, mafunzo, kuwa na uchumi wa kidigitali na siasa bora, mambo ambayo Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuyatekeleza.

Katika tukio jingine, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango namekutana na mkufanya mazungumzo na Waziri wa Ushirikianao wa Biashara wa Finland, Mhe.  Ville Skinnari, ambapo walijadili mambo mbalimbali yakiwemo masuala ya ushirikiano na maendeleo ya kiuchumi.

No comments:

Post a Comment