NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amesema juhudi zinazofanywa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Wadau wa utalii nchini ni moja ya hatua muhimu ya kuihamasisha jamii kuona thamani ya kutembelea vivutio vya Utalii vilivyopo nchini badala ya kutegemea Watalii kutoka nje.
Aidha, Mhe.Kanyasu amesema juhudi hizo zinaenda sambamba na kuhamasisha jamii kushiriki moja kwa moja katika shughuli za kiuchumi katika maeneo ambako shughuli za kitalii zinafanyika badala ya kudhani kuwa Watalii wanaokuja kwa ajili ya kutembelea vivutio vya Utalii wanakuja kwa ajili ya kuhodhi njia za kiuchumi
Akizungumza leo na Watalii wa ndani wapatao 100 katika kisiwa cha Sinda kilichopo katika wilaya ya Kigamboni Jijin Dare s Salaam, Mhe.Kanyasu amesema kuimarika kwautalii wa ndani kutaifanya jamii kuwaona Watalii wa kutoka nje ya nchi ni fursa kutokana na mzunguko wa pesa kutoka kwa Watalii kwenda kwa jamii.
Katika Tamasha hilo la kuhamasisha Utalii wa ndani wa ndani lililowakutanisha Manaibu Waziri watatu akiwemo Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu, Naibu Waziri wa Mambao ya Nje na Ushirikiano wa Kikanda, Dkt. Damas Ndumbaro pamoja na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega
Mhe. Kanyasu amesisitiza " Tunataka jamii ikiona Mtalii ameibiwa au ameporwa jamii isikitike na kuona fursa za kiuchumi zinatoweka kupitia mtalii aliyetendewa vibaya''
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kikanda, Dkt.Dramas Ndumbaro amesema sekta ya Utalii ni sekta mtambuka na Watalii wanapotembelea vivutio vya Utalii jamii nzima inafaidika
Kutokana na hilo, Naibu Waziri Ndumbaro ameitaka jamii kuacha kuposti vitu visivyofaa kwenye mitandao ya kijamii vya kuichafua nchi badala yake jamii itangaze vivutio vya Utalii vilivyopo nchini.
" Tangazeni vivutio vya Utalii ili watu wa nje waweze kufahamu vivutio vyetu vilivyopo nchi ni" alisisitiza Dkt.Ndumbaro.
Naye, Naibu Waziri wa Kilimo na Mifugo, Mhe.Abdallah Ulega amesema Utalii wa fukwe ni utajiri wa Watanzani wote hivyo jamii ijitokeze kutembelea fukwe hizo.
Amesema ni muhimu jamii kuona ufahari wa kutembelea visiwa vilivyotunzwa kwa ajili ya kupumzika na kujiburudisha baada ya kukamilisha majukumu mazito ya kila siku.
Naye, Mmiliki wa Siga tours and Travel Agency ambaye ni Muaandaji wa Tamasha hilo la Utalii wa ndani, Emma Sizzya ametoa wito kwa Wadhamini wenye ni ya kudhamini matamasha ya Utalii wa ndani wajitokeze kusaidia hili kuhamasisha Utalii wa ndani.
" Sisi hatuhitaji fedha tunachohitaji ni utayari wako kusaidia ili kuamsha ari ili jamii iweze kuhamasika na Utalii wa ndani, alisisitiza Muaandaji wa Tamasha hilo, Emma Sizzy
" Sisi hatuhitaji pesa tunachohitaji kutoka kwa Wadhamini ni msaada wa kile anachozalisha kitakachosaidia kufanikisha tamasha la Utalii kuweza kufanyika
No comments:
Post a Comment