HABARI-KAYA MASIKINI NGORONGORO ZAPATIWA MBUZI 624 - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 19 February 2020

HABARI-KAYA MASIKINI NGORONGORO ZAPATIWA MBUZI 624


Baadhi ya mbuzi na kondoo

Na Ahmed Mahmoud,Arusha


Kaya masikini zinazoishi katika kata ya Olbalbal wilayani Ngorongoro  zimepatiwa mbuzi na kondoo 624  watakaowasaidia kupunguza kiwango cha umasikini na kujipatia mahitaji muhimu pamoja na kujiendeleza kiuchumi.

Wananchi hao kutoka kaya zenye kipato duni wakizungumza katika makabidhiano ya mbuzi  hao waliotolewa na kikundi cha Narikungishu kilichopo  boma la utamaduni la ,Indemwa lililopo katika kata hiyo ,John Ngeka na Nalepo Emanuel walisema   kuwa mifugo hiyo itawawezesha kupata kipato cha uhakika ,licha ya kutegemea shughuli za ufugaji na utalii wa utamaduni bado wataongeza kipato chao kupitia ufugaji.

John Ngeka alisema kuwa atatumia mbuzi hao na kondoo katika kuongeza tija ya ufugaji na kujipatia kipato kutokana na mifugo kwa ili aweze kubadilisha maisha yake na familia yake.

Diwani wa kata hiyo Emmanuel Tonge  alisema kuwa kwa kipindi cha mwaka jana walitoa mbuzi 300 lakini kwa mwaka huu wametoa mbuzi 624 ili kuinua kipato cha maisha ya kaya masikini ziweze kujimudu na kukua kiuchumi.

"Mbuzi hawa na kondoo tunawagawa kwa kaya masikini ili ziweze kujikwamua kiuchumi badala ya kuwapa fedha tunawapa mifugo ili waweze kuifuga izaliane na kuongezeka na kuwaongezea kipato kitakachowainua kiuchumi" alisema Emmanuel

Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Rashid Taka alisema kuwa licha ya uwezeshaji huo wanapaswa kulinda utamaduni wao ambao umekua chanzo cha utalii kupitia utalii wa utamaduni na kuonya baadhi ya watu wanaoiba utamaduni na ubunifu na kuufanya bila kufuata sheria na taratibu .

Taka aliyataka maboma ya utamaduni kuiga mfano wa boma hilo kwa kuwawezesha  wananchi wanaozunguka kata hiyo ili waweze kunufaika na matunda ya utalii wa utamaduni.

No comments:

Post a Comment