WATU wawili wamegundulika kuwa na virusi vya corona nchini Uingereza, mkuu wa idara ya afya nchini humo ametangaza.
Hakuna taarifa iliyotolewa zaidi kuhusu familia hiyo na wapi wanapopatiwa matibabu.
Takriban watu 213 nchini china wamepoteza maisha kutokana na virusi hivyo, hasa kutoka mjini Hubei, huku kukielezwa kuwa na watu 10,000 walioathirika nchi nzima.
Watu 98 wamegundulika kuwa na virusi katika nchi nyingine 18.
Shirika la afya duniani limetangaza mlipuko wa virusi vya corona ni janga duniani.
Kwa sasa, raia 83 wa Uingereza na 27 wa mataifa ya kigeni wanarejea Uingereza kutokea Wuhan, mji ambao ni kitovu cha mlipuko nchini China.
Abiria hao watawekwa karantini katika hospitali ya Arrowe Park kwa majuma mawili.
-BBC
No comments:
Post a Comment