Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe (Kushoto) akibadilishana nyaraka za mashirikiano na Mwanasheria wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Kelvin Rogers. TBS itasaidia kutoa elimu kwa wajasiliamali na Wafanyabiashara kuzalisha na kuhifadhi nafaka kwa kuepuka sumukuvu.
KATIBU Mkuu Wizara ya Kilimo Mhandisi
Mathew Mtigumwe amewatakawashaurielekezi waliosaini mikataba ya
kusanifumiundombinu kwa ajili ya
utekelezajimradi wa kudhibiti Sumukuvu (TANIPAC) kuifanya kazi hiyo kwa weledi
na ubora.
Ametoa kauli hiyo jana Jijini Dodoma
wakati wa hafla ya kusainimikataba mitatu na Makampuniyenye thamani ya Shilingi
Milioni 868.7 ,randama mbili za mashirikiano
na taasisi za TBS na VETA kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa kudhibiti
Sumukuvu nchini.
“Mfanye kazi kwa weledi sana, sasa
Wizara ya Kilimo tunazingatia weledi.Hatutamvumiliamshaurielekezimzembe
,tutawasimamia kwa karibu na kuhakikisha thamani ya fedha inaonekana kwenye
miradi hii ya kudhibiti sumukuvu” alisema Mhandisi Mtigumwe.
Kampuni zilizosaini mikataba ni M/S
Digital Space kusanifukarantine ya maabara ya utafiti wa magonjwa ya
kibaiolojia,Sundy Merchant Ltd kufanyatahthmini ya awali ya mradi wa Sumukuvu
na A.V Consult kufanyausanifu na ujenzi wa maghala 14 ya hifadhi ya mahindi na
karanga.
Aidha, Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya UfundiStadi(VETA)imesaini
randama ya mashirikiano ya kufundishavijanamafundimchundo 400 kutengeneza teknolojia
ya kuhifadhi mazao wakati Shirika la Viwango (TBS) limeingia makubaliano na Wizara
ya Kilimo kusaidia kutoa elimu kwa wajasiliamali na Wafanyabiashara kuzalisha
na kuhifadhi mazao kwa kuepuka sumukuvu ili wapatesoko la uhakika na salama
katika mnyororo wa thamani ya mazao nchini.
Akizungumza wakati wa utiajisaini Mkurugenzi
Mkuu wa VETA nchini Dkt.PancrasBujulu alisema ni fursa
nzuriwamepatakufundishamafundimchundokutengeneza vihengerahisi kwa ajili ya
kuhifadhi mazao ya wakulima ilikulindaafya za watu kwa kutumia teknolojia bora.
“Ni
wajibu wetu VETA kutoa mafunzo kwa vijana nchini ili wazalishe vifaa bora
(vihenge) kwa ajili ya kuhifadhi nafaka na kujipatiaajira” Dkt.Bujulu alisema.
Aliongeza kusema vijanahawa 400 toka
wilaya 18 za Tanzania Bara watakuwachachu ya kusambazateknolojia hii rahisi na
bora ya uhifadhi nafaka nchini. Mratibu wa mradi wa kudhibiti Sumukuvu
(Tanzania Iniatives for Preventing Aflatoxin Contamination-TANIPAC)
ClepinJosephat alisema mradi huu wa miaka mitano(2019-2023)unatekelezwa nchini
kwa lengo la kuhakikisha usalama wa chakula hususan kwenye mazao ya mahindi na
karangahayachafuliwi na fangasiwanaosababisha sumukuvu.
Aliongeza kusema sumukuvu tangu
ilipogunduliwa nchini imesababisha madhara kwa wananchi ikiwemokuongezeka kwa
uwezekano wa kansa ya ini,udumavu kwa watoto chini ya miaka 5 na vifo.
Katika mwaka 2016 jumla ya watu 19
walikufa na wengine 68waliugua nakulazwakutokana na sumukuvuaina ya Aflatoxin
kwenye mikoa ya Dodoma na Manyara ambayo imeathirika zaidi.
No comments:
Post a Comment