Mhe. Innocent Bashungwa Waziri wa Viwanda na Biashara akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoa Mwanza
amekitembelea kwa mara ya pili kiwanda cha Mwatex (2001) LTD kilichobinafisiswa na Serikali kwa
mwekezaji Amin Radhanin na chenye wafanyakazi 600.
Kwenye ziara ya kwanza ya tarehe 30/09/2019 alitoa maelekezo kwa kiwanda kuhusu kuandaa mpango
mkakati wa biashara wa kuendesha kiwanda lakini mpaka sasa huo mpango mkakati haujafika wizarani.
Waziri baada ya kufika kiwandani hapo aliomba uongozi na menejiment nzima kutoka nje na mkutano ili
kusikiliza kero na changamoto pia na maoni yao yatakayofanya kiwanda hicho kinafanye kazi kwa
asilimia 100.
Amabapo kwa sasa kinafanya kazi asilimia 60 tofauti na matalajio ya serikali ya kiwanda
kufanya kazi kwa asilimia 100
Waziri baada ya kusikiliza maona na kero za wafanyakazi ameagiza wizara kuunda kamati maalum
ambayo itafika kiwandani kufanya uchambuzi wa uendeshaji wa kiwanda kwa kushirikiana na msimazi
anaekiendesha kiwanda hicho na amewapa muda mpaka 01/01/2020 kamati hiyo iwe imeshamfikishia
ripoti ya uchambuzi wa mwenendo wa kiwanda cha Mwatex
Ripoti hiyo itaisaidia serikali kupata mwelekeo wa nini kifanyike ili kupata Mwatex iliyokuwepo enzi za
Mwalimu Nyerere.
Pia Waziri amesisitiza kuwa mkakati wa serikali ni kuona viwanda vyote vinafufuliwa na vinafanya kazi ili
serikali iweze kutengeneza mnyororo wa thamani ya mazao yote hapa nchini.
No comments:
Post a Comment