Baadhi ya Maofisa wa Shirika la Posta na waandishi wa habari, wakiwa katika mkutano wa uzinduzi wa shindano hilo la kuadhimisha miaka 40 ya Umoja wa Posta Afrika, jijini leo.
Meneja Mkuu Rasilimali za Shirika, Macrice Mbodo, akizungumza katika uzinduzi huo.
Baadhi ya Maofisa wa Shirika la Posta wakifuatilia uzinduzi wa shindano hilo, la kuadhimisha miaka 40 ya Umoja wa Posta Afrika.
Kaimu Postamasta Mkuu, Mwanaisha Ali Said, akizungumza wakati akizindua shindano hilo, jijini leo.
Kaimu Postamasta Mkuu, Mwanaisha Ali Said (katikati), akitoa maelezo ya shindano la uandishi wa makala kwa waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo.
Baadhi ya Maofisa wa Shirika la Posta wakimsikiliza Kaimu Postamasta Mkuu, Mwanaisha Ali Said, alipokuwa akizungumza katika uzinduzi huo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Elia Madulesi, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika mkutano huo.
Meneja Mkuu Rasilimali za Shirika, Macrice Mbodo, akijibu maswali ya waandishi wa habari katika mkutano wa uzinduzi wa shindano hilo.
SHIRIKA la Posta lilikuwa na mkutano na waandishi wa habari kuzindua Shindano Maalum la Uandishi wa Makala. Shindano hilo ni maalum katika kuadhimisha siku ya Posta Afrika. Umoja wa Posta Afrika - PAPU tarehe 18 january, 2020 utaadhimisha miaka 40 tangu Shirikisho hilo la Posta Afrika lilipoanzishwa mwaka 1980.
Katika kuadhimisha siku hiyo, PAPU kwa kushirikiana na TPC imeandaa shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na Shindano la uandishi wa makala. Shindano hilo linashirikisha waandishi wa habari na wanafunzi wa vyuo wanaosoma taaluma ya uandishi wa habari.
Maadhimisho hayo yataambatana na shughuli za ugawaji wa vyeti na zawadi mbalimbali kwa washindi (10) watakaoshinda katika shindano la uandishi wa makala. Makala moja bora miongoni mwa washindi watatu itasomwa mbele ya Mgeni Rasmi Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa maadhimisho hayo ya miaka 40 ya Umoja wa Posta Barani Afrika (PAPU), yatakayofanywa Jijini Arusha tarehe 18 January 2020.
Malengo ya shindano hilo ni kukuza vipaji, kuchangia utengamano wa elimu ngazi ya kitaifa na kimataifa, kukuza uwezo wa kufikiri,kutafakari na kuhamasisha waandishi wa habari ili kupata uelewa zaidi juu ya maswala mtambuka na muhimu ya kitaifa.
Mada ya shindano hilo ni; “Andika makala ukieleza umuhimu wa anwani za makazi na misimbo ya posta (post code) katika kujenga Tanzania ya viwanda” au kwa kiingereza “Write an article explaining the importance of phyisical adressing and Postcode in building an industrilized Tanzania”.
Urefu wa makala: Makala ziwe na maneno kati ya 1000-2000. Utahitajika kuonyesha anwani yako sahihi ikiwa na e-mail pamoja na namba yako ya simu na jinsia.
Zawadi zitakazotolewa kwa washindi wa shindano hilo ni kompyuta mpakato, “smart phone”, “digital camera”, fedha taslimu na vyeti.
Shindalo hili linaanza rasmi leo tarehe 11 Disemba, 2019 na kuhitimishwa tarehe 31 Disemba, 2019.
Makala hizo zitumwe kwa njia ya EMS kwa anwani ifuatayo; Meneja Masoko, Shirika la Posta Tanzania, jengo la “Posta House”, 7 Mtaa wa Ghana, S. L. P 9551, 11300 Dar es Salaam.
IMETOLEWA NA; OFISI YA UHUSIANO POSTA MAKAO MAKUU
DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment