RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AONGOZA WATANZANIA KATIKA MAPOKEZI YA NDEGE MPYA YA BOMBARDIER ILIYOWASILI JIJINI MWANZA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 14 December 2019

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AONGOZA WATANZANIA KATIKA MAPOKEZI YA NDEGE MPYA YA BOMBARDIER ILIYOWASILI JIJINI MWANZA


Picha mbalimbali zikionesha Ndege hiyo ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza wakati ikitokea nchini Canada. PICHA NA IKULU.

Ndege mpya aina ya DE Havilland DASH8-400 ikipokelewa kwa saluti ya maji na Kikosi cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ilipotua Uwanja wa Ndege wa Mwanza ikitokea Canada na kupokelewa na maelfu ya wananchi wakiomngiozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Jumamosi Desemba 14, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Balozi wa Canada nchini Mhe. Pamela O'Donell na viongozi wengine akikata utepe kuashiria kuipokea rasmi ndege mpya ya DE Havilland DASH8-400 katika uwanja wa Ndege wa Mwanza Jumamosi Desemba 14, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapongeza kwa furaha marubani wazalendo walioendesha ndege mpya ya DE Havilland DASH8-400 kutoka Canada na kutua salama katika uwanja wa Ndege wa Mwanza Jumamosi Desemba 14, 2019.


Picha mbalimbali zikionesha Ndege hiyo ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza wakati ikitokea nchini Canada. PICHA NA IKULU.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua ndege hiyo mara baada ya kuwasili.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameketi na Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ndani ya  ndege mpya iliyonunuliwa na Serikali aina ya Bombardier Q400 mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Mwanza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wafanyakazi wa ATCL wakati wa mapokezi ya  ndege mpya ya DE Havilland DASH8-400 kutoka Canada na kutua salama katika uwanjawa Ndege wa Mwanza Jumamosi Desemba 14, 2019.

No comments:

Post a Comment