KWANDIKWA AKAGUA ATHARI ZA MAFURIKO LUSHOTO, AAGIZA NGUVU IONGEZWE UJENZI WA BARABARA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 18 December 2019

KWANDIKWA AKAGUA ATHARI ZA MAFURIKO LUSHOTO, AAGIZA NGUVU IONGEZWE UJENZI WA BARABARA

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias John Kwandikwa akitoa maelekezo alipokuwa akikagua athari za mafuriko Wilayani Lushoto.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias John Kwandikwa akitoa maelekezo alipokuwa akikagua athari za mafuriko Wilayani Lushoto.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias John Kwandikwa akikagua athari za mafuriko Wilayani Lushoto na kutoa maelekezo anuai.

Matengenezo yakiendelea kwa sehemu zilizoathiriwa na mafuriko Wilayani Lushoto.

Matengenezo yakiendelea kwa sehemu zilizoathiriwa na mafuriko Wilayani Lushoto.

Naibu Waziri Kwandikwa akikagua athari za mafuriko Lushoto na kuangalia ujenzio unaofanyika mara baada ya athari za mvua.

NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias John Kwandikwa amekagua athari za mafuriko wilayani Lushoto, huku akiagiza nguvu iongezwe ujenzi wa barabara ya Lushoto-Mlalo.

Alisema Serikali imejipanga kuhakikisha barabara yote ya Lushoto-Mlalo KM 48 inajengwa kwa kiwango cha lami. Pamoja na hayo amesisitiza kuwa barabara zote wilayani Lushoto zilizobomoka kutokana na mvua kubwa iliyonyesha zitajengwa haraka ili kuhakikisha haziathiri huduma za kijamii na kiuchumi.
Naibu Waziri Kwandikwa yuko katika ziara ya siku tatu kukagua athari za mafuriko mkoani Tanga.

No comments:

Post a Comment