IROLE FC YAPOKEA KIPIGO CHA 6-1KUTOKA KWA MAFINGA ACADEM KATIKA ASAS SUPER LEAGUE 2019/2020 - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 3 December 2019

IROLE FC YAPOKEA KIPIGO CHA 6-1KUTOKA KWA MAFINGA ACADEM KATIKA ASAS SUPER LEAGUE 2019/2020

Waamuzi wa Asas Super League 2019/2020 ambao wamekuwa wakichezesha michezo mingi ya ligi hiyo yenye msisimko mkoani Iringa na nje ya mkoa wa Iringa (picha kutoka maktaba).

Mwenyekiti wa chama cha mpira mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava akiwa wasalimia wachezaji wa timu ya Irole fc waliofungwa sita moja na timu ya Mafinga Academy (picha kutoka maktaba).

NA FREDY MGUNDA,IRINGA

TIMU Irole FC ya wilayani kilolo mkoani Iringa imekuwa timu ya kwanza kupata kipigo kikubwa kuliko timu zote zinazoshiriki ligi ya Asas Super League 2019/2020 baada ya kupokea kipigo cha goli sita kwa bila.

Timu ya Irole fc inayoshikili nane bora ya Asas Super League imejikutaka ikikung’utwa goli sita moja na timu ya Mafinga Academy katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Wambi uliopo katika uwanjwa wa wilaya ya Mufindi.

Ikumbukwe kuwa Irole fc ndio moja ya timu bora kabisa kushiriki ligi hiyo huku wakionyesha upinzani mkubwa kwenye hatua za awali za ligi hiyo ambao moja ya mechi ambazo walicheza kwa kutoa vipigo vingi huku kipigo kikubwa kikiwa kwenye mchezo wao dhidi ya Ismani fc ambao waliwabugiza tano mchezo ulichezwa kwenye nuwanja wa Irole fc.

Tangu timu ya Irole fc itinge hatua ya nane bora tayari imeshacheza michezo mitatu huku ikitoa sare michezo miwili huku mmoja akipokea kipigo kikali kutoka kwa Mafinga Academ

Katika michezo ambayo imechezwa siku hii ya leo timu ya Ismani Fc imeendeleza ubabe wake kwa kuitungua goli moja timu ya kimali fc kutoka katika uwanja wa kijiji cha ruang’a kilichopo tarafa ya Ismani mkoani Iringa.

Na michezomingine itaendelea siku ya kesho kati ya Nzihi fc ambao watakuwa wanawakaribisha timu ya Mkimbizi fc kutoka manispaa ya Iringa na mchezo huo utachezwa katika uwanja wa kijiji cha Nzihi.

No comments:

Post a Comment