Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), George Simbachawene akifungua Maonesho ya 14 ya Kitaifa ya Siku ya Nishati Jadidifu yaliyofanyika Mnazi Mmoja, Dar es Salaam. |
Makamu Mwenyekiti wa TAREA, Mhandisi Prosper Magali(kulia) akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa Maonesho ya 14 ya Kitaifa ya Siku ya Nishati Jadidifu yaliyofanyika Mnazi Mmoja, Dar es Salaam. |
Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Jeroen Verheul akizungumza kwenye uzinduzi wa Maonesho ya 14 ya Kitaifa ya Siku ya Nishati Jadidifu yaliyofanyika Mnazi Mmoja, Dar es Salaam. |
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), George Simbachawene akiangalia majiko yaliyotengenezwa kitaalamu kulinda mazingira na yanatumia mkaa na kuni. |
*Ataka
mataifa yasimwage Tv na Friji mbovu Afrika
WAZIRI wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), George Simbachawene,
ameiagiza Jumuiya ya Wadau wa Nishati Jadidifu Tanzania (TAREA) kufanya
utafiti katika Jiji la Dar es Salaam ili kubaini kiasi cha matumizi ya nishati
jadidifu.
Alitoa
agizo hilo wakati akifungua Maonesho ya 14 ya Kitaifa ya Siku ya Nishati Jadidifu
yaliyofanyika Mnazi Mmoja, Dar es Salaam yakiwa na kauli mbiu: “NISHATI JADIDIFU KUFIKIA TANZANIA YA VIWANDA 2025”
yaliyoandaliwa na TAREA na kufanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar Salaam.
Aidha,
ameyataka mataifa yaliyoendelea kuacha kuleta bidhaa chakavu za kielektroniki
zikiwamo runinga na friji katika nchi zinazoendelea ikiwamo Tanzania kuacha kwa
kuwa ni majanga.
Alikuwa
akijibu risala ya TAREA iliyosomwa kwake na Makamu Mwenyekiti wa TAREA,
Mhandisi Prosper Magali aliyesema licha ya TAREA na wadau mbalimbali
kuhamisisha matumizi teknolojia ya nishati jadidifu, zipo changamoto kubwa za
kudhibiti taka zitokanazo na bidhaa za kielektroniki zikiwamo runinga na friji.
Simbachawene
alisema inasikitisha kuona vifaa vilivyotumika na kuchakaa katika mataifa
yaliyoendelea bado zikiwamo friji na TV bado zinaletwa katika mataifa
yaliyoendelea ikiwamo Tanzania.
Akasema:
“Kwa nchi zilizoendelea, kama kitu ni kibaya, tusikitumie wote; tusione ni
kibaya tukapeleka Afrika maana madhara yake tabaka la ozini ni
makubwa. Uchafuzi wa hali ya
hewa husababisha kumomonyoka kwa tabaka la ozoni na
kubadilika kwa tabianchi huathiri watui wote.”
Alisema
serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira, imeandaa kanuni mpya za
udhibiti na usimamizi wa taka hatarishi za mwaka 2019 zilizoanza kutumika
Septemba mwaka huu.
“Kanuni
hizi zinasimamia taka hatarishi mbalimbali zikiwamo betri chakavu, hivyo
serikali inawahakikishia kuwa itaendelea kusimamia kanuni hizo ipsavyo ili
kudhibiti uchafuzi unaoweza kutokea na utupaji usio salama,” alisema na
kuongeza kuwa, matumizi ya niashati ya kuaminika na endelevu hayaepukiki kwa
maendeleo ya taifa na kuelekea uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025.
Simbachawene
alisema: “Mafanikio katika sekta zote za uchumi, huduma za jamii na maendeleo
yanategemea upatikanaji wa kuaminika na endelevu wa nishati ya kutosha usiokuwa
na madhara katika mazingira.”
Alisema
sekta ya viwanda kutumia fursa hiyo kujipatia umeme katika vyanzo vya nishati
safi na nafuu kwa shughuli za viwanda kwa mifumo na kazi kama kuchemsha mahji,
kuvuta maji kwa ajili ya umwagiliaji na majiko sanifu kwa taasisi za umama kama
shule na majeshi.
“Natoa
mwito kwa taasisi za umma kama majeshi, magereza, hospitali, shule na vyuo
kuingia katika matumizi ya teknolojia ya nishati jadidifu maana miti mingi
inakatwa na magereza na shule hivyo, uharibifu wa mazingira ni mkubwa…,”
alisema.
Balozi wa
Uholanzi nchini Tanzania, Jeroen Verheul alisema ili teknolojia ya nishati
jadidifu isambae na kutumika zaidi kwa umma, lazima kuwepo mazingira rafiki
zaidi ya kisera na kisheria na kwamba, sula hjili linahitahji ubia wa dhati.
Alisema
nchi yake itaendelea kushitrikiana na Tanzania katika kusaidia matumizi ya
teknolojia ya nishati jadidifu am,bayo ni msaada katika mapambano ya kidunia
dhidi ya majanga yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi.
Awali,
Mhandisi Magali ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa TAREA na Mwenyekiti wa Kamati ya
Maandalizi ya maonesho hayo, alimwambia waziri kuwa, licha ya TAREA na wadau
mbalimbali kuhamisisha matuimizi yteknolojia ya nishati jadidifu, zipo
changamoto kubwa za kudhibiti taka zitokanazo na bidhaa za kielektrponiki
zikiwamo runinga na friji.
“Taka za
kielektroniki zimeendelea kuongezeka na tupo kwenye hatari kubwa ya uchafuzi wa
mazingira kupitia taka hizi,” alisema magali.
Akaongeza:
“Tunaomba Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira kukamilisha utungaji wa sheria za
kusimamia biashara ya taka za kielektroniki ili kuwezesha shughuli za urejelezaji wa
taka hizo ili kuhifadhi mazingira.”
No comments:
Post a Comment