Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza wakati wa kikao cha kusikiliza kero za wafanyaabiashara wa Jiji la Tanga kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi akizungumza wakati wa kikao hicho.
Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure akizungumza wakati wa kikao hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga katikati akisisitiza jambo akiwa na Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure kulia na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said kushoto wakati wa kikao hicho.
Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim kulia akiwa kwenye kikao hicho.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Edward Bukombe kushoto akiwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa wakifuatilia kikao hicho.
MENEJA wa Benki ya NMB Tawi la Mkwakwani Jijini Tanga akifuatilia kikao hicho.
Wadau mbalimbali wakifuatilia kikao hicho wakiwemo wafanyabiashara kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu.
Elirehema Kimambo ni Meneja Msaidizi Ukaguzi wa Kodi TRA Mkoa wa Tanga akati wa kikao hicho na kushoto ni Meneja Msaidizi Madeni ya Kodi TRA Mkoa wa tanga Lucas Kaigarula.
Wadau mbalimbali wakifuatilia kikao hicho wakiwemo wafanyabiashara kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu.
RC Shigella aliyasema hayo leo wakati wa kikao cha kusikiliza kero za wafanyaabiashara wa Jiji la Tanga kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huku akieleza pia kwamba serikali haiwezi kujitegemea iwapo watu hawataridhia kulipa kodi bila kushurutisha.
Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi,Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa,Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji,wafanyabiashara na viongozi mbalimbali.
Mkuu huyo wa mkoa alisema kwamba pia serikali haiwezi kujitegemea iwapo watu hawataridhia kulipa kodi bila kushurutishwa huku akisisitiza kwamba kazi kubwa anayoifanya Rais Dkt Magufuli ni kuhakikisha anasimamia mapato yanakusanywa.
Alisema kwamba serikali ina matarajio makubwa kwamba nchi katika misingi imara iliyoasisiwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ya dhana ya kujitegemea kwamba watanzania wanajitegemea wenyewe kwenye mipango yao, kuitekeleza na kuifanisi.
Aidha alisema watanzania wanajitegemea kwenye kutekeleza mipango yao na kufanikisha na moja ya chanzo cha cha mapato ni kuhakikisha kodi inalipwa na ndio maana serikali ya Rais Dkt John Magufuli imeweka jitihada zake kubwa katika kuhakikisha watanzania tunajitegemea.
“Lakini pia hatuna mjomba mwengine ambaye tunaweza kumuomba msaada na Serikali ya awamu ya tano sio ya kupiga magoti na rais wetu tunamfahamu matumaini yake macho yake yapo kwa watanzania kuhakikisha wana simamia miradi”Alisema.
Alisema miradi yote mkubwa inayoendelea inahitaji fedha ili iweze kujiendesha na hilo linatokana na watanzania kulipa kodi hivyo watambue kwamba kuna umuhimu wa kufanya hivyo.
Anasema kuioa ulipa kodi ndio wanaona ujenzi wa barabara ya poangani Tanga mkandarasi amekabidhiwa eneo na wiki ijayo ili barabara hiyo iweze kutengenezwa, bandari ya Tanga ilikuwa na tatizo la muda mrefu tayari ufumbuzi wake umanza kupatikana kuna mashine majini inachimba kina kutoka cha sasa mpaka kufikia mita 14 hadi 15 ili kuruhusu meli zinazokwenda Dar ziwezi kufika Tanga.
Awali akizungumza wakati wa kikao hicho Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure alisema kikao hicho kinakatokana na agizo la Naibu Kamisha wa TRA Msafiri Mbibo ambaye aliagiza kuandaa kikoa kingine ambacho kitajumuisha mamlaka hiyo na taasisi nyengine zinazohusika na wafanyabiashara.
Alisema kikao hicho ni kutiia agizo la Naibu Kamishna huyo ambapo Mkuu huyo wa mkoa alihaidi kwamba atakuwa mgeni rasmi kusimamia na kusikiliza kero za wafanyabiashara hao.
No comments:
Post a Comment