Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Hemed Suleiman akiweka alama ya
vidole wa ajili ya usajili laini ya simu katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada
katika Viwanja vya Gombani Mjini Pemba.
MKuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Hemed Suleiman akikabidhiwa
kitabu cha Muongozo wa Mawasiliano na Mkuu
wa Kanda ya Zanzibar wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Esuphatie
Masinga (katikati) wakati wa Kampeni ya a Mnada kwa Mnada wa TCRA katika
Viwanja vya Gombani Mjini Pemba. Kushoto ni Mkuu wa Kanda ya Mashariki TCRA
Mhandisi Lawi Odiero na watatu kutoka kushoto Afisa Habari Mwandamizi wa TCRA
Makao Makuu Mabel Masasi.
Afisa Habari wa TCRA Judith Shao akitoa maelezo kuhusiana
vitabu vya Muongozo wa Mawasiliano Katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada katika
Viwanja vya Gombani Mjini Pemba.
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Hemed Suleiman ameipongeza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kwa kuandaa kampeni ya Mnada kwa Mnada kwa kuwa inasaidia sana wananchi kupata huduma kirahisi.
Mkuu huyo ameyasema
hayo wakati wa Kampeni ya Mnada kwa Mnada wa TCRA katika Viwanja vya Gombani Mjini
Pemba amesema kwa kusogeza huduma
zote muhimu pamoja inawarahisishia wananchi kupata huduma jambo ambalo
linamanufaa kwa wananchi na serikali kwa ujumla.
Hemed Amewataka wananchi kutumia vema fursa ya kampeni huyo inapofika katika maeneo yao. Kampeni ya Mnada kwa Mnada
Pemba katika utoaji wa Elimu ya Usajili
wa laini kwa kutumia alama za vidole.
Wakazi wa wilaya ya Pemba na viunga vyake wamejitokeza kwa
wingi katika kampeni ya Mnada kwa Mnada
ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu,
Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Idara ya Uhamiaji kwa ajili ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho
vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa
laini za simu.
Kampeni tangu imeanzishwa imekwenda katika Mikoa 17 na
Zanzibar lengo kuu ni nchi nzima kufikiwa na Kampeni hiyo. Mkuu wa TCRA Zanzibar
Esuphatie Masinga amesema ni fursa kwa wananchi wa Pemba kufika katika Viwanja
vya Gombani kwa ajili ya kusajili kwa alama za vidole pamoja na kujiandikisha
kupata usajili wa vitambulisho vya Taifa kutokana na kuwa na mnyororo wadau
wa mawasiliano.
Masung amesema kuwa Mnada kwa Mnada TCRA ilianzisha ili
kutoa fursa ya Wananchi kuhudumiwa hasa wakati huu usajili wa laini za simu kwa
alama za vidole pamoja Huduma zingine za mawasiliano.
Aidha amesema Kampeni hiyo ni kuimarisha ulinzi katika huduma
za simu pamoja kufanya mawasiliano kuwa salama katika nchi. Mkuu huyo amesema
kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya
mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto wanazokutanazo
katika utumiaji wa mawasiliano nchini.
Masinga amesema kuwa
wananchi wasio kuwa na Vitambulisho vya NIDA wahakikishe wanapata katika usajili wa laini za simu kwa
kutumia alama za vidole na huduma nyinginezo za Mawasiliano hayo.
Hata hivyo amesema kuwa kuna watu wengine wanatumia
mawasiliano ya simu bila kujua ambapo Jeshi Polisi lipo katika Kampeni ya Mnada
kwa Mnada ili kutoa elimu kuhusiana
makosa ya jinai ya matumizi ya simu.
Aidha amesema Kampeni hiyo ni endelevu katika kuwafikia
ikiwa kuhakikisha kila mwananchi anajisajili laini yake kwa alama za vidole kwa
kutumia kitambulisho cha taifa. TCRA iko kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi ili watumie
Mawasiliano kwa usalama kutokana na elimu wanayoipata katika Kampeni
mbalimbali. Hata hivyo amesema kuwa wananchi wajitokeze katika kujisajili kwa
alama za vidole kabla ya Desemba 31.
"TCRA
tunawafikia katika wananchi katika utoaji wa elimu za utumiaji wa bidhaa
za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo" amesema Masinga.
Naye Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TCRA Mabel Masasi
amesema kuwa mwitikio umekuwa mkubwa kwa Wananchi kutaka vitambulisho kwa ajili
ya kusajili laini za simu kwa alama za vidole na kupata mwamko wa kutumia simu
katika maendeleo.
Masasi amesema kuwa Wananchi wa watumie Kampeni ya Mnada kwa
Mnada ya TCRA kupata elimu na baada ya kuisha Mnada sehemu husika waende katika
mamlaka husika kupata vitambulisho.
Wananchi wakipata maelezo kuhusiana na usajili kwa alama za
vidole katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada Viwanja vya Gombani Mjini Pemba.
No comments:
Post a Comment