Mwenyekiti wa Mtaa wa Benue, James Manakila akiwatambulisha Wajumbe wa mtaa wake kwa Mbunge wa Geita mjini Mhe.Constantine Kanyasu. |
MBUNGE wa Geita mjini na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ameanza kuwatambulisha Wenyeviti wateule wa Chama cha Mapinduzi( CCM) kwa wananchi kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii.
Akizungumza na Wananchi wa eneo la Mpomvu katika Kata ya Mtakuja mkoani Geita, Mhe.Kanyasu ametumia fursa hiyo kuelezea mafanikio yaliyopatikana katika katika kipindi chake cha Uongozi wa miaka minne.
Katika mkutano huo, Mhe.Kanyasu amewatambulisha Wenyeviti wateule wa mitaa saba kwa wananchi na kuwataka watoe ushirikiano ili kuleta maendeleo. Ametaja mafanikio hayo kuwa yamepatikana katika nyanja ya Elimu, Afya, Barabara, mikopo pamoja na Umeme.
Mbali ya kuelezea mafanikio hayo yaliyopatikana katika utekezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM (2015-2020) katika jimbo hilo, Mhe.Kanyasu ametaka wananchi kutoa ushirikiano kwa Wenyeviti wapya watakaopatikana katika uchaguzi huo ili kuharakisha miradi ya maendeleo.
Baadhi ya wananchi walioshiriki mkutano wa Hadhara wa Mbunge wa Geita mjini, Mhe.Constantine Kanyasu wakati wa kiwatambulisha viongozi wateule wa CCM. |
No comments:
Post a Comment