KAMPENI YA MNADA KWA MNADA YA TCRA YAINGIA MKOANI SINGIDA, NI KUTOA ELIMU YA USAJILI WA LAINI KWA ALAMA ZA VIDOLE - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 21 November 2019

KAMPENI YA MNADA KWA MNADA YA TCRA YAINGIA MKOANI SINGIDA, NI KUTOA ELIMU YA USAJILI WA LAINI KWA ALAMA ZA VIDOLE

Mkuu wa Kanda ya Kati wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Anthony Manyanda akizungumza na Wananchi wakati wa utoaji wa elimu ya usajili wa laini za Simu kwa alama za vidole wakati wa Kampeni ya Mnada Kwa Mnada iliyofanyika Viwanja vya Stendi ya Zamani ya mabasi mkoani Singida.

Afisa Habari Mwandamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mabel Masasi akitoa elimu ya usajili wa laini za Simu kwa alama za vidole ikiwa ni Kampeni ya Mnada kwa Mnada iliyofanyika Viwanja vya Stendi ya Zamani ya mabasi mkoani Singida.

Mtoa wa huduma wa Kampuni ya Simu za Mkononi akimsajili mwananchi kusajili laini ya simu kwa alama za vidole katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada iliyofanyika Viwanja vya Stendi ya Zamani ya mabasi mkoani Singida.

Wananchi wakiwa wamepanga foleni kwa ajili ya kuangalia namba ya vitambulisho katika mfumo wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada iliyofanyika Viwanja vya Stendi ya Zamani ya mabasi mkoani Singida.

WAKAZI wa Mkoa Singida na viunga vyake wamejitokeza kwa wingi katika kampeni ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Idara ya Uhamiaji kwa ajili ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.

Kampeni hiyo tangu imeanzishwa imekwisha ifikia Mikoa 18, huku lengo kuu ikiwa ni kufanyika nchi nzima kutoa elimu hiyo.

Mkuu wa Kanda ya Kati wa TCRA, Anthony Manyanda amesema ni fursa kwa wananchi wa Mkoa Singida kufika Stendi ya zamani ya mabasi kwa ajili ya kusajili kwa alama za vidole pamoja na kujiandikisha kupata usajili wa vitambulisho vya Taifa kutokana na kuwa na mnyororo wadau wa  mawasiliano.

Manyanda amesema kuwa Mnada kwa Mnada TCRA ilianzisha ili kutoa fursa ya Wananchi kuhudumiwa hasa wakati huu usajili wa laini za simu kwa alama za vidole pamoja Huduma zingine za mawasiliano.

Manyanda amesema Kampeni hiyo ni kuimarisha ulinzi katika huduma za simu pamoja kufanya mawasiliano kuwa salama katika nchi na kuongeza kuwa muda ni huu na kuacha kusubiri mwisho wa mwezi Desemba.

Amesema kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano nchini.

Manyanda amesema kuwa wananchi wasio kuwa na Vitambulisho vya NIDA wahakikishe wanapata ili waweze kusajili laini za simu kwa kwa alama za vidole na huduma nyinginezo za Mawasiliano hayo.

Hata hivyo amesema kuwa kuna watu wengine wanatumia mawasiliano ya simu bila kujua ambapo Jeshi Polisi lipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ili kutoa elimu kuhusiana makosa ya jinai ya matumizi ya simu yasiofuata sheria.

Aidha amesema Kampeni hiyo ni endelevu katika kuwafikia ikiwa kuhakikisha kila mwananchi anajisajili laini yake kwa alama za vidole kwa kutumia kitambulisho cha taifa. Amesema TCRA iko kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi ili watumie Mawasiliano kwa usalama kutokana na elimu tunayotoa.

Hata hivyo amesema kuwa wananchi wajitokeze katika kujisajili kwa alama za vidole kabla ya Desemba 31 na muda uliobakia ni mdogo tangu tangazo lilipotolewa.

"TCRA tutahakikisha tunawafikia katika wananchi katika utoaji wa elimu za utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo," amesema Manyanda.

Manyanda amesema kuwa Kampeni hiyo imeanza kwa Mikoa yote iliyopo katika kanda ya Kati.

Naye Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TCRA, Bi. Mabel Masasi amesema kuwa mwitikio umekuwa mkubwa kwa Wananchi kutaka vitambulisho kwa ajili ya kusajili laini za simu kwa alama za vidole.
Masasi amesema kuwa Wananchi wa watumie Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA kupata elimu na baada ya kuisha Mnada sehemu husika waende katika mamlaka husika kupata vitambulisho.

No comments:

Post a Comment