Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias John
Kwandikwa akisitiza jambo kwa mkandarasi GS Eng
& Const. na wasimamizi wanaojenga daraja jipya la Selander lenye
urefu wa mita 1030 na barabara unganishi zenye urefu wa KM 5.2 jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias John Kwandikwa akisitiza jambo kwa
mkandarasi GS Eng & Const. na wasimamizi
wanaojenga daraja jipya la Selander lenye urefu wa mita 1030 na barabara
unganishi zenye urefu wa KM 5.2 jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias John Kwandikwa akimwelekeza jambo
mmoja wa wasimamizi wanaosimamia ujenzi wa daraja Jipya la Selander lenye urefu
wa mita 1030 na barabara unganishi zenye urefu wa KM 5.2 jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias John Kwandikwa akisisitiza jambo
kwa Eng. Samson Kundineza alipokuwa akikagua ujenzi wa daraja Jipya la Selander
lenye urefu wa mita 1030 na barabara unganishi zenye urefu wa KM 5.2 jijini Dar
es Salaam.
Kazi ya ujenzi wa nguzo za daraja
jipya la Selander lenye urefu wa mita 1030 zikiendelea jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias John Kwandikwa akizungumza na
waandishi wa habari mara baada ya kukagua ujenzi daraja Jipya la Selander lenye
urefu wa mita 1030 na barabara unganishi zenye urefu wa KM 5.2 jijini Dar es
Saam.
NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias John Kwandikwa ameelezea kuridhishwa
kwake na maendeleo ya ujenzi wa daraja jipya la Selander lenye urefu wa mita
1030 na barabara unganishi zenye urefu wa KM 5.2 jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
mara baada ya kukagua ujenzi huo leo, amempongeza mkandarasi GS Eng &
Const. kutoka Korea Kusini na wasimamizi wanaojenga daraja hilo kwa kasi
inayoendana na makubaliano ya mkataba.
“Nawapongeza
kwa kazi nzuri inayoendelea katika ujenzi wa mradi huu na nawaagiza wataalam
wote wa wizara wanaoshiriki katika mradi kujifunza kikamilifu ili tupate hazina
ya wataalam wengi zaidi,” amesisitiza Naibu Waziri Kwandikwa.
Kwa upande
wake Msimamizi wa Ujenzi huo, Eng. Lee Suk Joo amesema wamejipanga kuhakikisha
ujenzi wa mradi huo unakamilika kwa wakati kwa kuzingatia ubora na pia kuongeza
idadi ya wataalamu wa madaraja haoa nchini.
Daraja jipya
la Selander lenye urefu wa mita 1030 na upana wa mita 20.5 litakalo kuwa na
njia nne za magari, njia za watembea kwa miguu pamoja na barabara unganishi
zenye urefu wa KM 5.2 linataraajiwa kukamilika mwaka 2021 na kupunguza kiasi
kikubwa msongamano wa magari katikati ya jijini la Dar es Salaam.
Imetolewa na Kitengo cha Habari na
Mawasiliano Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

No comments:
Post a Comment