![]() |
| Mbunge wa Jimbo la Mtama (CCM), Nape Moses Nnauye akiwa Ikulu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli alipokwenda kumuomba msamaha kwa kumkosea. |

NAPE AMUOMBA MSAMAHA RAIS
MAGUFULI IKULU…!
MBUNGE
wa Jimbo la Mtama (CCM), Nape Moses Nnauye leo amefika Ikulu na kuomba
msamaha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli kwa
yote aliyomkosea. Hata hivyo Rais Magufuli ametangaza kumsamehe mbunge huyo
machachari wa CCM na kumtaka aendelee kuchapa kazi kwa kuwatumikia watanzania
katika nafasi alizonazo.
Akizungumza
Ikulu mara baada ya mazungumzo na mbunge Nape, Rais Dk Magufuli alisema amekuwa
akipokea ujumbe mfupi mara kadhaa wa mbunge huyo akiomba kusamehewa kwa popote
alipoteleza.
Aidha Rais
Magufuli amesema amemsamehe kwa moyo mweupe kwa kuwa yeye kama binadamu wengine
wamefundishwa kusamehe kiimani, hivyo hawezi kuendelea kuweka kinyongo moyoni
hata kama alimkosea.
Nape sasa
anaingia kwenye orodha ya wanasiasa wenzake vijana, yaani January Makamba na William
Ngeleja ambao nao waliamua kujirudi na kumuomba msamaha rais kwa makosa waliomkosea,
ambao nao Rais Magufuli alitangaza kuwasamehe kwa moyo mweupe.

No comments:
Post a Comment