NA MWANDISHI WETU
WADAU wa masuala ya
Wanawake na Watoto wamekutana ili kujadili na kufanya tathimini ya Utekelezaji
wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto
(MTAKUWWA) kwa kipindi cha robo ya kwanza 2019/2020.
Akizungumza wakati
akifungua kikao kazi hicho cha siku mbili kuanzia Septemba 18 hadi 19, 2019
kilichofanyika katika Ukumbi wa Bwalo la JKT UMWEMA mkoani Morogoro Mratibu wa
Taifa wa Mpango huo Bi. Happiness Mugyabuso amesema, Serikali kwa kushirikiana
na Washirika wa Maendeleo wameandaa kikao kazi hicho ili kujadili na kufanya
tathimini ya utekelezaji wa Mpango Kazi huo.
“Leo
tumekutana hapa kwa pamoja kwa lengo la kufanya tathimini ya utekelezaji wa
mpango kazi huo katika kipindi cha robo ya kwanza kwa Mwaka 2019/2020.
Aliongezea kuwa, pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika robo ya kwanza ya
utekelezaji wa Mpango Kazi, kikao kazi kitajadili pia changamoto zilizojitokeza
katika kipindi husika na kuweka mikakati mahsusi ya kuimarisha utekelezaji wake
kwa vipindi vya robo zinazofuata,”alisema Bi. Happiness.
Aidha
kikao hicho kilitoa fursa ya kujadili namna bora ya kuboresha mfumo wa
ukusanyaji na uchakataji wa taarifa za takwimu za utekelezaji wa MTAKUWWA ili
kuimarisha upatikanaji wa takwimu za msingi (baseline data). Hatua
hii ni muhimu kwani itasaidia kupima hali ya utekelezaji wa Mpango Kazi katika
vipindi mbalimbali vikiwemo vya mwaka na miaka mitano (5).
Mmoja
wa washiriki wa kikao hicho Bw.Emmanuel Burton ambaye ni Afisa Maendeleo ya
Jamii kutoka Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii alieleza kuwa, Miongoni mwa maeneo
yaliyojadiliwa ni pamoja na namna bora ya upatikanaji wa taarifa sahihi za
utekelezaji katika sekta mbalimbali ambazo zinatekeleza mpango huo na kuwa na
mikakati ya namna ya kuwafikia walengwa kikamilifu ili kukidhi lengo mpango
ifikapo mwaka 2021/ 2022.
“Kikao
kazi hiki ni muhimu kwa kuzingatia kuwa, malengo mahsusi ya utekelezaji wa
Mpango wa MTAKUWWA yanajadiliwa na kuhakikisha tunaandaa taarifa sahihi zenye
tija kuhusu makundi hayo ili vita dhidi ya ukatili wa wanawake na watoto
inapiganwa na kuleta matokeo chanya,”alisema Burton
No comments:
Post a Comment