MARAIS MUSEVENI, MAGUFULI WAFUNGUA KONGAMANO LA KIBIASHARA LA TANZANIA NA UGANDA DAR - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 7 September 2019

MARAIS MUSEVENI, MAGUFULI WAFUNGUA KONGAMANO LA KIBIASHARA LA TANZANIA NA UGANDA DAR


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Dkt John Pombe Magufuli akihutubia wakati wa ufunguzi wa kongamano la kwanza la kibiashara kati ya Tanzania na Uganda lililofanyika jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo limewashirikisha wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda huku wakiongozwa na marais Dkt John Pombe Magufuli na Mhe. Yoweri Museveni. Picha zote na Matokeo Chanya+.

Wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda wakifuatilia hotuba za marais wa Tanzania na Uganda.

Rais wa Uganda Rais Yoweri Museveni akihutubia wakati wa ufunguzi wa kongamano la kwanza la kibiashara kati ya Tanzania na Uganda lililofanyika jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo limewashirikisha wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Dkt John Pombe Magufuli akifuatilia hotuba ya Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Museveni wakati wa ufunguzi wa kongamano la kwanza la kibiashara kati ya Tanzania na Uganda lililofanyika jijini Dar es Salaam.

Wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda wakifuatilia.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Palamagamba Kabudi akiwakaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Dkt John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Museveni wakati wa ufunguzi wa kongamano la kwanza la kibiashara kati ya Tanzania na Uganda lililofanyika jijini Dar es Salaam. 


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Palamagamba Kabudi.

Mtukio mbalimbali katika mkutano huo.

No comments:

Post a Comment