TAASISI isiyo ya kiserikali ya Vodacom Tanzania Foundation (VTF) leo imesaini mkataba wa makubaliano na WWF (World Wide Fund for Nature) ili kuchangia milioni 303 kwa ajili ya mradi wa “kijanisha Dodoma” ambao umeratibiwa na ofisi ya makamu wa rais kwa kushirikiana na WWF. Hafla hiyo ya usainishaji ilifanyika leo katika ofisi za WWF jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na Afisa wa Mazingira kutoka ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dr Thomas Bwana aliyemwakilisha Mgeni rasmi naibu katibu mkuu katika Wizara hiyo Mheshimiwa Balozi Joseph Sokoine..
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Dr Bwana amesifu mpango wa Vodacom Tanzania Foundation na WWF (World Wide Fund for Nature) kupambana na hali ya mabadiliko ya tabia nchi. Pia aliongeza kuwa amefurahi namna makampuni na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yanavyoungana kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu namba 13 juu ya hali ya hewa.
“Kutokana na asilimia 80 ya watu kutegemea mazingira na maliasili kwa ajili ya kutengeneza kipato, kulinda maliasili ni jambo muhimu litakalochochea mafanikio ya kufikia mpango wa maendeleo ya kiuchumi. Serikali imeweka mikakati kwa ajili ya kupambana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi nchini Tanzania pamoja na kuhakikisha kuwa jamii inamifumo ya kukabiliana na mabadiliko haya, jambo linalofanya tufurahie ushirikiano huu.”
Aidha Dk Bwana aliongeza kuwa serikali ina mpango wa kupanda miti milioni 280 kila mwaka ili kuunga mkono mpango wa taifa wa kusimamia na kupanda miti kwa ajili kuifanya nchi yetu kuwa ya kijani.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation Rosalynn Mworia, amesema kuwa wamefurahia kuingia ubia na WWF ili kutekeleza mpango huo ambao unawiana na mpango mkakati wa VTF kwa mwaka 2019/21 ambao umejikita katika kuchochea hatua za kudhibiti mabadiliko ya tabia nchi.
Kama kampuni ya Vodacom, maono yetu ni kuwaunganisha watu ili kuleta maendeleo Tanzania, tuna matumaini ya kuunda jamii ya kidijitali, tukilenga kujenga uchumi jumuishi na kufanya kazi katika sayari ambayo athari zetu ni ndogo. Mradi huu umejidhatiti katika kuifanya Dodoma kuwa ya kijani lakini tunatumaini uwepo wa ongezeko la hatua za kisasa dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi kutoka ufahamu na uhamasishaji wa jamii,” alisema Mworia.
Akizungumzia ushirikiano huo, Mkurugenzi mkazi wa WWF Tanzania, Dr Amani Ngusaru amesema kuwa mfuko huo utaelekezwa kuunga mkono juhudi za serikali katika kuufanya mji wa Dodoma kuwa kijani kwa kupanda miti 100,000 kwa mwaka wa kwanza na kutengeneza bustani ndani ya mji mkuu pamoja na kuongeza ufahamu na kuhamasisha jamii kwa kuwapa mafunzo makundi ya vijana na wanawake katika uzalishaji na matumizi ya mifuko ya plastiki mbadala na kusimamia taka kama shughuli ya kuwawezesha kiuchumi.
Tumejidhatiti kuunda miradi endelevu ambayo itasaidia kudhibiti changamoto za kimazingira na kijamii nchini Tanzania. Tunaishukuru Vodacom Tanzania Foundation kwa kutuunga mkono katika kutekeleza mpango huu. Athari za mabadiliko ya tabia nchi zinaonekana katika maeneo mbalimbali nchini, hivyo kurejesha mfumo wa ikolojia na kulinda maliasili ni njia mahususi ya kuzuia madhara yenye uwezo wa kuharibu maisha ya watu na utekelezaji wa mradi huu utakuwa ni hatua kubwa sana katika kushughulikia changamoto hizo,” aliongeza Dr Ngusaru.
Mradi huo uliopewa jina “kuishi kwa amani na mazingira asili” utaanza rasmi mwezi Septemba mwaka huu na utatekelezwa kwa kushirikiana na ofisi ya makamu wa rais – mazingira, halmashauri ya jiji la Dodoma na taasisi ya huduma za misitu (TSF)
Ends-
About WWF
WWF is one of the world’s largest and most respected independent conservation organizations, with over 5 million supporters and a global network active in more than 100 countries and territories. WWF's mission is to stop the degradation of the Earth's natural environment and to build a future in which humans live in harmony with nature, by conserving the world's biological diversity, ensuring that the use of renewable natural resources is sustainable, and promoting the reduction of pollution and wasteful consumption. Visit www.panda.org/news for the latest news and media resources.
About Vodacom Tanzania Foundation
The Vodacom Tanzania Foundation helps vulnerable groups across the country improve their health, access better education, promote sustainable environment and agriculture. Working with local NGOs and partners, Vodacom Tanzania Foundation has supported over 120 projects to date investing over Tsh 15 Bn to improve the lives of those in Tanzania. For further information, please visit: https://vodacom.co.tz/en/vodacom_foundation_aboutus/
Vodacom Tanzania Foundation is one of a network of global and local social investment programmes linked to the Vodafone Foundation. Vodafone Foundation’s Connecting for Good programme combines charitable giving and technology to make a difference in the world.
No comments:
Post a Comment