Sehemu ya washiriki wa Mkutano mkuu wa mwaka wa dharura wa TCCIA mwaka 2019 unaofanyika New African Hotel Jijini Dar es salaam wakifatilia hotuba ya waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, leo tarehe 24 Agosti 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akifungua Mkutano mkuu wa mwaka wa dharura wa TCCIA mwaka 2019 uliofanyika New African Hotel Jijini Dar es salaam, leo tarehe 24 Agosti 2019.
Sehemu ya washiriki wa Mkutano mkuu wa mwaka wa dharura wa TCCIA mwaka 2019 unaofanyika New African Hotel Jijini Dar es Salaam wakifatilia hotuba ya waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, leo tarehe 24 Agosti 2019.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es Salaam
SERIKALI imesema kuwa imejipanga lkuongeza ushirikiano na Sekta binafsi katika kuhakikisha kuwa kero na vikwazo vinaondolewa
ili kuweka mazingira bora ya biashara na kuvutia uwekezaji wa ndani na nje ya nchi.
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 24 Agosti 2019 wakati
akimuwakilisha Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa kufungua Mkutano mkuu wa mwaka
wa dharura wa TCCIA mwaka 2019 huku akiongeza kuwa serikali imefanya uamuzi mahususi
mwaka huu wa kuondoa muingiliano wa utoaji wa huduma za mashirika ya TBS na TFDA ili kupunguza
usumbufu kwa Wanyabiashara.
Alisema
kuwa hizo ni hatua za awali na ametoa mwito kwa TCCIA kuhakikisha kuwa wafanyabiashara
wanafuata sheria, kanuni na taratibu zote zilizowekwa ili kuondoa usumbufu wote
unaoweza kujitokeza wakati wa kufanya biashara.
Alisema kuwa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli alizindua Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Kilimo (ASDP
II) tarehe 4 Juni, 2018. Kwa kutambua umuhimu wa Sekta Binafsi, moja ya
maboresho makubwa ya ASDP II ukilinganisha na ASDP I ni kuipa nafasi kubwa
zaidi Sekta Binafsi.
Aliongeza kuwa ni wakati
muafaka wa kubaini maeneo maalumu ambayo Taasisi hiyo ya TCCIA itaendelea kutoa
mchango mkubwa katika kutekeleza programu hiyo ili iweze kufikia malengo
yaliyowekwa.
Mhe Hasunga amesema kuwa ili
kuhakikisha uboreshaji wa Mazingira ya biashara nchini, Serikali kwa
kushirikiana na Sekta Binafsi iliandaa andiko maalumu “Blue Print” ambalo lilikwisha zinduliwa, pia mpango wa utekelezaji
wake umeandaliwa na umeanza kutekelezwa.
“Ni wajibu sasa wa kila pande
yaani Sekta ya Umma na Binafsi kuhakikisha kuwa yale yote yaliyoainishwa katika
andiko hilo yanatekelezwa ipasavyo” Alikaririwa Mhe Hasunga
Vile vile, amesema kuwa
serikali imeendelea na jitihada za kuimarisha Mabaraza ya Biashara ya Mikoa na
Wilaya ambapo tayari imeshaweka Mwongozo wa Mabaraza hayo ambayo TCCIA ni
Sekretarieti.
Waziri Hasunga amewataka
washiriki hao kuchangamkia fursa
zilizopo katika miradi mikubwa inayotekelezwa na Serikali nchini, hasa miundo
mbinu ya reli ya Kisasa, mradi wa umeme wa bwawa la Nyerere, barabara za kisasa,
bomba la mafuta, manunuzi ya ndege n.k.
Alisema kuwa Fursa hizo kwa
kupitia sera ya “Local Content” nao wakiwa wazawa wana nafasi kubwa ya
kunufaika nazo.
Amesema, Miradi hiyo ni mingi
na itachukua muda mrefu ikitekelezwa kwa awamu tofauti. “Endapo kwa sababu moja
au nyingine haukuweza kupata fursa ya kushiriki kazi kwenye mradi mmoja kwa
sababu fulani zikiwemo sifa kadhaa basi, nakushauri ujipange vizuri kwenye
miradi inayokuja, msikate tamaa” Alisisitiza Mhe Hasunga
Alisema
kuwa serikali inatambua ushirikiano mzuri wa TCCIA na taasisi mbali mbali za Umoja
wa Mataifa (UN) zikiwemo UNDP, UNIDO, FAO, UNV, UNESCO, ILO, na ITC, pamoja na Wadau
wengine wa kimaendeleo kama Trade Mark East Africa.
Ushirikiano
huo kwa kupitia mifumo ya kielektroniki ya kuripoti na kufuatilia vikwazo mbalimbali
(NTBs Reporting and Monitoring System) na utoaji wa vyeti vya Uasili wa Bidhaa
kwa njia ya kielektroniki (Electronic Certificates of Origin) umesaidia sana
uondoaji wa vikwazo vya biashara visivyokuwa vya kiforodha (NTBs).
Pia,
TCCIA imeshirikiana na Wadau wengine kama vile VSO, ENGEN, USAID, East African
Trade Hub, BMZ, KOICA, JICA, TRIAS na DANIDA kupitia Local Investment Climate
(LIC) kuimarisha biashara na mfumo wa majadiliano na sekta ya umma. Kwa kipekee
ninawapongeza sana kwa mashirikiano hayo.
No comments:
Post a Comment