NAIBU SPIKA DKT TULIA AKSON AWASILISHA KWA NIABA YA SPIKA MAMBO 15 YALIYOFANYWA NA RAIS MAGUFULI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 26 August 2019

NAIBU SPIKA DKT TULIA AKSON AWASILISHA KWA NIABA YA SPIKA MAMBO 15 YALIYOFANYWA NA RAIS MAGUFULI

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dkt Tulia Akson akipokelewa katika uwanja wa Majengo mjini Moshi na baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro pamoja na serikali wakati wa Kongamano la Wanawake  lililofanyika mkoani Kilimanjaro akimwakilisha Spika Job Ndugai.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dkt Tulia Akson akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Chama na Serikali alipowasili katika viwanja vya Majengo mjini Moshi kwa ajili ya Kongamano la Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) lililofanyika mjini Moshi mwishoni mwa wiki.

Naibu Spika wa JAmhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Tulia Akson akizungumza katika Kongamano hilo.

Baadhi ya Wanawake kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kilimanjaro wakifuatilia hotuba mbalimbali zilizotoklewa katika kongamano hilo.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka akizungumza katika kongamano hilo.

Baadhi ya  Wanawake katika kongamano hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Dkt Anna Mghwira ambaye alikuwa mwenyeji wa kongamano hilo akieleza juu ya miradio mbalimbali iliyotekelezwa katika mkoa wa Kilimanjaro ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020.

Baadhi ya Viongozi wa Taasisi mbalimbali za serikali wakiwa katika Konagamano hilo.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro ,Patrick Boisafi akizungumza katika kongamano hilo.

Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Kilimanjaro Zuhura Chikira akizungumza katika Kongamano hilo.


Naibu Waziri wa Nishati, Mh Subila Mgalu akiwaeleza washiriki wa Kongamano hilo namna ambavyo utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ulivyofanyika katika sekta ya Nishati. 

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa akiwaeleza washiriki wa Kongamano hilo namna ambavyo njia ya Treni ya kutoka Tanga kuja Kilimanjaro ilivyofanyiwa marekebisho ili kurahisisha usafirishaji wa mizigo na mipango ya baadae ya shirika hilo.

Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa, Esther Mmasi akizungumza katika Kongamano hilo.

Mkuu wa wilaya ya Same, Rosemery Senyamule akizungumza katika Konagamano hilo.

Burudani ya muziki kutoka Bendi ya Chuo cha Polisi iliwakusanya wanawake hao kucheza muziki katika ya uwanja.

Na Dixon Busagaga, Moshi 
SPIKA wa Bunge, Job Ndugai, ametaja mambo 15 aliyofanya Rais John Magufuli kwa kipindi cha miaka minne alichokaa madarakani na kuwataka watanzania kumuunga Mkono.
Ndugai ameyataja mjini Moshi, wakati wa kongamano la kumpongeza Rais lililoandaliwa na Umoja wa wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT).
Hotuba ya Ndugai ilisomwa kwa niaba yake na Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Akson , katika uwanja wa Majengo na kuhudhuriwa na wanachama wa UWT na wanawake wa mkoa huo.
Ndugai alisema  Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015-2020, imetekelezwa kwa kiwango kikubwa,na kwamba miongoni mwa mambo ambayo ametekeleza Rais ni kurejesha nidhamu kwa watumishi.
Alisema lingine ni kushughulikia tatizo sugu la Rushwa ndani ya serikali,na ndani ya chama cha mapinduzi hali ambayo itapunguza kwa kiasi kikubwa rushwa ya uchaguzi katika Chaguzi zijazo.
Akizungumza mwenyekiti wa UWT Taifa, Gaudensia Kabaka, alisema kongamano hilo lililenga kumpongeza Rais kwa kazi kubwa aliyoifanya katika kipindi cha miaka minne na kwamba mambo makubwa yamefanyika katika kipindi hicho.

Mwisho

No comments:

Post a Comment