MCHUNGAJI MKOANI SINGIDA APIGWA BUTWAA NA KAZI ZA RAIS DKT.JOHN MAGUFULI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 8 August 2019

MCHUNGAJI MKOANI SINGIDA APIGWA BUTWAA NA KAZI ZA RAIS DKT.JOHN MAGUFULI

 Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la FPCT Utaho (B) Yungi, Francis Pius akiongoza ibada iliyofanyika Jumapili katika kanisa hilo lililopo Puma wilayani Ikungi mkoani Singida.


Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu, akivikwa skafu baada ya kuwasili katika kanisa hilo kushiriki ibada hiyo.

 Watoto wa kanisa hilo wakiwa ibadani.

 Waumini wa kanisa hilo wakiwa ibadani.

 Waumini wa kanisa hilo wakiwa ibadani.

 Wake wa viongozi wa kanisa hilo wakiwa kwenye ibada hiyo.

 Mbunge Kingu akizungumza kwenye ibada hiyo.

 Mchungaji Pius na viongozi wengine wa kanisa hilo wakiwaombea Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi,Elibariki Kingu na Katibu wake Njou Muna katika ibada hiyo.

 Kaimu Mtendaji wa Kijiji cha Utaho B,  ambaye ni muumini wa kanisa hilo, Paul Singi akizungumza.

 Viongozi wa kanisa hilo wakiwa ibadani. Kutoka kushoto ni Mchungaji Mathayo Trotimi, Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo, Francis Pius na Mchungaji Elisha Ngoi.

 Mbunge Kingu (wa pili kushoto), akiwa katika ibada hiyo. Kutoka kushoto ni Katibu wa Mbunge Njou Muna, Mzee wa Kanisa hilo, Ayubu Kisuda na Dereva wa Mbunge, Yusuf Daffi.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Utaho ambaye pia ni Muumini wa Kanisa hilo, Saimon Andalu akizungumza.


 Kwaya ya Vijana ya kanisa hilo, ikitoa burudani.

Mbunge Kingu, akitoa msaada wa sh.50,000 kwa bibi huyo kwa ajili ya kununulia sare za shule za mjukuu wake.


Na Dotto Mwaibale, Singida

MCHUNGAJI Kiongozi wa Kanisa la FPCT la Utaho (B) Yungi, lililopo Puma wilayani Ikungi mkoani Singida, Francis Pius amesema anapigwa  butwaa kwa kasi ya kazi za maendeleo zinazofanywa na Rais Dkt.Johnn Magufuli hapa nchini.

Mchungaji Pius aliyasema hayo katika ibada ya Jumapili iliyofanyika katika kanisa hilo na kuhudhuriwa na Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu.

"Kwa kweli Rais wetu Dkt. John Magufuli ananifanya nipigwe na butwaa kwa kazi kubwa anazozifanya za kutuletea maendeleo kwani katika miaka minne ya uongozi wake tumeona kazi nyingi zikifanyika hakika ni Rais wa wanyonge" alisema Mchungaji Pius.

Akizungumza katika ibada hiyo, Kingu aliwashukuru viongozi wa dini kwa umoja wao wa kumuombea Rais Dkt. John Magufuli na viongozi wengine na Taifa kwa ujumla na kuifanya nchi kuwa na amani na utulivu.

" Ninyi viongozi wa dini mnafanya kazi kubwa ya kuifanya nchi yetu kuwa na amani kutokana na maombi yenu ya kumuombea Rais wetu pamoja na Taifa mungu awabariki sana" alisema Kingu 

Akizungumzia shughuli za maendeleo zinazofanyika hapa nchini tangu Rais Magufuli achaguliwe kuongoza nchi alisema inatokana na Rais Magufuli kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za Serikali na kuzielekeza kufanya miradi ya maendeleo ya nchi.

" Kwa kweli Rais wetu amebana matumizi yasio ya lazima ya fedha za Serikali na hata sisi wabunge tangu achaguliwa hatujawahi kuongezwa mshahara na wala hatujawahi kusafiri kutoka nje ya nchi bila ruhusa yake" alisema Kingu.

Alisema katika kipindi cha miaka minne Rais Magufuli ameweza kununua ndege ambazo wanapanda watalii na kupata fedha za kigeni, ujenzi wa mradi wa umeme Rufiji, Ujenzi wa Reli ya treni ya mwendo kasi kutoka Dar es Salaam hadi Makutopora Dodoma, miradi ya maji, ujenzi wa zahanati na vituo vya afya, barabara, shule na miradi mingine mingi.

Alisema kazi hizo zote zinafanyika kutokana na uzalendo mkubwa alionao Rais Magufuli kwa kuwatumikia wananchi wa Tanzania.

Katika ujenzi unaoendelea wa kanisa hilo, Mbunge  Kingu aliweza kuchangia sh.milioni mbili na laki moja kwa ajili ya kutengeneza madirisha.

No comments:

Post a Comment