Hospitali mpya ya St Monica iliyojengwa na Taasisi ya Kirua Children Care Foundation katika kijiji cha Marua, kata ya Kirua Vunjo Magharibi katika wilaya ya Moshi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dk Anna Mghwira akiwa ameongozana na Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia pamoja na Mwenyekiti wa Taasisi ya Kirua Children Care Foundation ,Padri Amedeus Macha wakielekea katika ufunguzi rasmi wa Hosptali hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dkt Anna Mghwira akitia saini katika kitabu cha wageni alipofika katika Hosptali hiyo kwa ajili ya ufunguzi.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kirua Children Care Foundation ,Padri Amedeus Macha akimueleza jambo mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Dkt Anna Mghwira wakati akitembelea vyumba vya kulaza wagonjwa katika Hosptali hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira akitizama baadhi ya mashine zilizoko katika Hospitali hiyo.
Padri Amedeus Macha akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira chumba maalumu kwa ajili ya wanawake kujifungulia.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira akikata utepe kuashiria kufunguliwa rasmi kwa Hospitali hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Dkt Anna Mghwira akitoa kitambaa kufungua jengo hilo la Hosptali ya St Monica.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Dkt Anna Mghwira akizungumza wakati wa ufunguzi wa Hospitali ya St Monica iliyopo jimbo la Vunjo wilaya ya Moshi.
Mbunge wa Jimbo la Vunjo, James Mbatia akizungumza katika hafla ya ufunguzi rasmi wa Hospitali ya St Monica.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kirua Children Care Foundation, Padri Amedeus Macha akizungumza katika ufunguzi wa Hosptli hiyo.
Na Dixon Busagaga, Kilimanjaro
MBUNGE WA Jimbo la Vunjo, James Mbatia ameshauri
kuanzishwa kwa Utalii wa Tiba (Medical Tourism) katika eneo linalozunguka
Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) ili kurahisha utoaji wa huduma
kwa wageni wanaopata matatizo wakati wa kupanda mlima Kilimanjaro.
Mbatia aliyasema hayo wakati wa ufunguzi rasmi
wa Hospitali ya St Monica iliyopo jirani na Hifadhi ya Taifa ya Mlima
Kilimanjaro katika kijiji cha Marua ,kata ya Kirua Vunjo Magharibi,katika
wilaya ya Moshi huku akiiomba serikali
kusaidia katika uboreshaji wa Miundombinu ya barabara.
Akizungumza
mara baada ya kufungua na kutembelea
maeneo mbalimbali ya Hospitali Hospitali iliyojengwa na Taasisi ya Kirua
Children Care Foundation Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna
Mghwira ameipongeza taasisi hiyo kwa kujenga Hosptali hiyo ambayo itasaidia
kupunguza changamoto za kiafya kwa wakazi wa maeneo hayo na mkoa wa Kilimanjaro
kwa ujumla.
.
Naye Mwenyekiti wa Taasisi ya Kirua Children Care Foundation
Padri Amedeus Macha amesema Hospitali hiyo itakayo kuwa na uwezo wa vitanda zaidi
ya 100 imelenga kutoa huduma za matibabu kwa wazee na watoto ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakitembea umbali
mrefu kufuata huduma za Afya.
Dkt.Bogias
Mwamgunda ni mwakilishi wa mganga mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro hapa akaeleza
namna ambavyo Hosptali hiyo itasaidia Wazee na watoto katika kupambana na
magonjwa yatokanayo na Baridi .
Taasisi
za Dini katika jimbo la Vunjo zimekuwa mstari wa mbele katika uwekezaji wa
masuala ya huduma za afya ,hali inayochangia urahishaji wa upatikanaji wa
matibabu tofauti na ilivyokuwa kwa kutembea umbali mrefu hasa nyakati za
mvua na usiku.
No comments:
Post a Comment