RAIS DK MAGUFULI AZINDUA HIFADHHI YA TAIFA YA BURIGI CHATO MKOANI GEITA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday 9 July 2019

RAIS DK MAGUFULI AZINDUA HIFADHHI YA TAIFA YA BURIGI CHATO MKOANI GEITA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla pamoja na viongozi wengine wakivuta  utepe kuashiria uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi (Burigi -Chato National Park) ilioyopo Chato mkoani Geita. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia sanamu ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere yenye ujumbe maalum kuhusu umuhimu wa utunzaji wa mazingira ya wanyama pori.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkuu wa Mkoa Mstaafu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu mara baada ya kumkabidhi Hundi ya Shilingi milioni kumi, kama shukrani katika mchango wake alioutoa katika utunzaji wa wa hifadhi mbalimbali ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Burigi (Burigi -Chato National Park) ilioyopo Chato mkoani Geita.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Chato kabla ya kuzindua Hifadhi ya Taifa ya Burigi (Burigi  -Chato National Park) ilioyopo Chato mkoani Geita. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Kikosi cha Jeshi Usu la kukabiliana na vitendo vya Ujangili pamoja na kulinda hifadhi za taifa kabla ya kuanza kwa  sherehe za uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi (Burigi -Chato National Park) ilioyopo Chato mkoani Geita.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka mara baada ya kuzindua Hifadhi ya Taifa ya Burigi (Burigi  -Chato National Park) ilioyopo Chato mkoani Geita.

No comments:

Post a Comment