Na Khalfan Said
MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi
ya Jamii (NSSF) wamewasogezea karibu huduma Wanachama wa Mifuko hiyo katika
msimu huu wa Maonesho ya 43 ya Bishara ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu
Sabasaba.
Wakizungumza leo Julai 2, 2019 kwa nyakati tofauti Wakurugenzi Wakuu wa Mifuko hiyo, Bw. Hoseah E. Kashimba
(PSSSF) na Bw. William Erio (NSSF) wamesema kuwa wameamua kufanya maonesho hayo
kwa kushrikiana ili kuwarahisishia Wanachama kupata huduma wanazohitaji wote
wakiwa kwenye banda namba 13 lililo mkabala na jingo la matangazo ndani ya
viwanja vya Sabasaba.
“Tukiwa
katika banda hili kwa kushirikiana na wenzetu wa NSSF ambao wao wanashughulika
na wafanyakazi kutoka Sekta Binafsi na sisi PSSSF tunahudumia wafanyakazi
kutoka Sekta ya Umma.”
Tumeona
tufanye maonesho haya pamoja kwa sababu ya kutoa elimu kwa wanachama kwa
urahisi zaidi hasa kwa vile hatuko katika ushindani kama ilivyokuwa hapo awali,
hii itasaidia kama Mwanachama anataka kujua taarifa kuhusu Mafao yake kama
anatoka Sekta binafsi ataelekezwa aende NSSF na kama anatoka Sekta ya Umma
ataelekezwa aende PSSSF, amefafanua Bw. Kashimba.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Bw. William Erio alisema “Baada ya
kuunganishwa Mifuko hapo mwaka jana bado watu hawajaelewa vema tofauti zilizopo
kwa hiyo wanakuja hapa kama banda pekee linalotoa huduma ya Hifadhi ya Jamii na
wakifika basi wanaelekezwa katika sehemu husika na kupata huduma wanayohitaji.”
Alisisitiza Bw. Erio.
Alisema
ni sehemu ambayo watu wanaweza kuja na kujibiwa maswali yote waliyonayo na kutatuliwa
kero zao.
Maonesho
hayo ya kila mwaka yamefunhguliwa rasmi leo Julai 2, 2019 na Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan na yanatarajiwa
kufikia kilele Jlai 13, 2019.
Bw. Erio (kushoto) na Bw. Kashimba wakibadilishana mawazo ndani ya banda hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Hoseah E. Kashimba, (kushoto), akimuhudumia Mwanachama wa Mfuko huo aliyetembelea banda namba 13 la Mfuko huo na ule wa NSSF.
No comments:
Post a Comment