NMB WASISITIZA MTOTO AKAUNTI NA CHIPUKIZI AKAUNTI SABASABA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday 4 July 2019

NMB WASISITIZA MTOTO AKAUNTI NA CHIPUKIZI AKAUNTI SABASABA

Meneja Mradi wa Uwajibikaji kwa Jamii, Bi. Lilian Kisamba akizungumza juu ya umuhimu wa kuwaandaa watoto kuwa na nidhamu katika matumizi ya fedha na kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba kwa malengo, akiwa ndani ya Banda la Benki ya NMB kwenye maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea Sabasaba Dar es Salaam.

Sehemu ya watoto wanaotembelea Banda la NMB wakichorwa nyuso zao baada ya kupata huduma na elimu ya masuala ya fedha.

Bi. Lilian Kisamba akifafanua jambo alipozungumzia umuhimu wa kuwaandaa watoto kuwa na nidhamu katika matumizi ya fedha na kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba kwa malengo, akiwa ndani ya Banda la Benki ya NMB kwenye maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea Sabasaba Dar es Salaam.

Sehemu ya watoto wanaotembelea Banda la NMB wakichorwa nyuso zao baada ya kupata huduma.

BENKI ya NMB imewashauri wazazi na walezi kuwafungulia watoto wao akaunti za watoto pamoja na Chipukizi akaunti kwa ajili ya kuwawekea akiba na kuwajengea utamaduni wa kujifunza usimamizi wa fedha zao kwa maisha bora ya baadaye.

Kauli hiyo imetolewa leo katika viwanja vya Sabasaba ndani ya Banda la Benki ya NMB kwenye Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Akizungumza Meneja Mradi wa Uwajibikaji kwa Jamii, Bi. Lilian Kisamba alisema akaunti hizo zinasaidia kuwaandaa watoto kuwa na nidhamu katika matumizi ya fedha na kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba kwa malengo.

Alisema elimu hiyo ikitolewa vizuri na mapema kwa watoto na jamii nzima inasaidia kupunguza umasikini kwani tutakuwa nafamilia zenye uelewa na matumizi sahihi ya fedha kimalengo.
"Hizi akaunti za wajibu mzazi au mlezi anaweza kuweka kiwango chochote kwenye akaunti ya mtoto hata shilingi 1000 kwa akiba ya mtoto wake...pia hazina gharama zozote za uendeshaji kama akaunti zingine.

Aidha aliongeza kuwa jamiii kwa ujumla ina kila sababu ya kuona umuhimu wa elimu ya masuala ya fedha kuenea kwa kiasi kikubwa na hata ikiwezekana Serikali kuifanya sehemu ya mtaala ili iwe ikimfikia kila mmoja na kujifunza kwa undani wajibu na mahitaji.

No comments:

Post a Comment