NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, MHE. CONSTANTINE KANYASU AWAONGOZA KUNDI LA WANAFUNZI 20 WANAOSOMEA UONGOZI KUTALII HIFADHI YA TAIFA YA TARANGIRE - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday 5 July 2019

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, MHE. CONSTANTINE KANYASU AWAONGOZA KUNDI LA WANAFUNZI 20 WANAOSOMEA UONGOZI KUTALII HIFADHI YA TAIFA YA TARANGIRE

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu (wa pili kulia) akizungumza na kundi la Wanafunzi 20 wanaosomea mafunzo ya Uongozi (Uongozi Executive Programme 2019, Postgraduate Diploma in Leadership) waliotembelea Hifadhi ya Taifa ya Tarangire katika mkoa wa Manyara kwa lengo kubwa la kuhamasisha Utalii wa Ndani pamoja na kuwafanya wanafunzi hao kuwa Mabalozi wa Utalii nchini. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Hifadhi hiyo, John Gala.

Baadhi ya wanafunzi hao wakisalimiana na watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Tarangille mara baada ya kuwasili makao makuu ya Hifadhi hiyo iliyopo katika mkoa wa Manyara.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akiwa na kundi la Wanafunzi 20 wanaosomea mafunzo ya Uongozi (Uongozi Executive Programme 2019, Postgraduate Diploma in Leadership) wakipewa maelezo kutoka kwa Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Tarangile, John Gala. wakati walipotembelea Hifadhi ya Taifa  iliyopo katika mkoa wa Manyara kwa lengo kubwa la kuhamasisha Utalii wa Ndani pamoja na kuwafanya wanafunzi hao kuwa Mabalozi wa Utalii nchini.

Baadhi ya makundi ya tembo ambayo yameponekana katika hIFADHI YA taifa ya Tarangilre wakati wanafunzi hao walipotembelea Hifadhi hiyo leo.

No comments:

Post a Comment