Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Tanzania Bara, Philip Mangula akihutubia juzi wilayani Ikungi mkoani Singida katika mkutano wa kuwapongeza Wana CCM wa Jimbo la Singida Mashariki kwa ushindi aliopata mgombea nafasi ya ubunge kupitia chama hicho kwenye uchaguzi mdogo, Miraji Mtaturu ambaye alipita bila ya kupingwa.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Tanzania Bara, Philip Mangula, akivikwa Skafu baada ya kuwasili wilayani Ikungi kwa ajili ya mkutano huo. |
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Tanzania Bara, Philip Mangula, akisaini kwenye kitabu cha wageni Ofisi ya CCM Wilaya ya Ikungi . Kulia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Mkoa wa Singida Yohana Msita na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi, Mika Likapakapa.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Tanzania Bara, Philip Mangula, akizungumza na Viongozi wa CCM Mkoa wa Singida . Kulia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Mkoa wa Singida Yohana Msita na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi, Mika Likapakapa.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Tanzania Bara, Philip Mangula akimtuza mmoja wa wasanii waliokuwa wakitoa burudani nje ya Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kabla ya kuanza kwa mkutano huo.
Wana CCM wakiwa kwenye mkutano huo wakiimba wimbo wa Taifa.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Tanzania Bara, Philip Mangula akiimbiwa wimbo maalumu.
Mbunge Mteule wa Jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtaturu akishukuru.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mkoa wa Singida, Aisharose Matembe akizungumza katika mkutano huo.
Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu akizungumza katika mkutano huo.
Mbunge wa Iramba, Mwigulu Nchemba akizungumza katika mkutano huo.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Tanzania Bara, Philip Mangula (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wabunge wa Mkoa wa Singida. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi, Mika Likapakapa.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Mkoa wa Singida Yohana Msita akizungumza.
Mke wa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Tanzania Bara, Philip Mangula, akisalimia. Kulia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Singida, Jane Kessy na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi, Mika Likapakapa.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi, Mika Likapakapa akizungumza.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Tanzania Bara, Philip Mangula, akimbidhi mbunge huyo mteule Miraji Mtaturu ilani ya uchaguzi ya chama hicho ya mwaka 2015/2020 ikiwa ni ishara ya kuanza kazi ya kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo la Singida Mashariki.
Na Dotto Mwaibale, Singida
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Tanzania Bara, Philip Mangula ametoa onyo kwa wanachama wa chama hicho kuanza kujipenyeza kwenye majimbo ili kuwania nafasi za ubunge na udiwani wakati majimbo hayo yakiwa na wawakilishi.
Mangula alitoa onyo hilo mwanzoni mwa wiki alipokuwa akizungumza na wana CCM wilayani Ikungi mkoani Singida katika mkutano wa kuwapongeza WanaCCM wa Jimbo la Singida Mashariki kwa ushindi aliopata mgombea nafasi ya ubunge kupitia chama hicho kwenye uchaguzi mdogo, Miraji Mtaturu ambaye alipita bila ya kupingwa.
" Natoa maelekezo kuwa mtu yeyote atakayebainika kuanza kujipenyeza kwenye majimbo kwa nia ya kuanza kufanya kampeni ya kuwania nafasi hizo za uongozi hatutamuonea huruma tunamchukulia hatua kali za kinidhamu" alisema Mangula.
Alisema katika majimbo hayo kuna wawakilishi ambao muda wao wa miaka mitano bado haujaisha hivyo waachwe watekeleze ilani ya chama hicho kwa kuwapelekea wananchi maendeleo.
Alisema mwana CCM mwenye nia ya kutaka nafasi hizo anatakiwa kusubiri muda utakapo fika na wanachotakiwa sasa ni kwenda kwa wananchi kutangaza kazi za maendeleo zilizofanywa na viongozi waliopo madarakani na si kuanza kuwania majimbo hayo
Mangula alitoa maagizo kwa wana chama hicho kuwa pindi watakapo muona mtu yeyote ameanza kujipenyeza katika majimbo hayo watoe taarifa ili mtu huyo aweze kuchukuliwa hatua kali kupitia kamati ya maadili.
Katika hatua nyingine Mangula alielezea umuhimu wa kutoa elimu ya mpiga kura ili kila mtu aweze kujua haki yake ya kikatiba ya kupiga kura.
Alisema katika uchaguzi mkuu uliopita katika baadhi ya maeneo watu waliojitokeza kupiga kura walikuwa wachache kutokana nakutokuwepo kwa elimu hiyo hivyo kujikuta kiongozi akichakuguliwa kwa kura chache akitolea mfano katika Jimbo la Igalula mkoani Tabora ambapo idadi ya wapiga kura walikuwa ni asilimia 22 kati ya watu 100.
"Kuna umuhimu mkubwa wa kutoa elimu hii walau mgombea aweze kupata zaidi ya asilimia 40 kuliko kuwa chini ya hapo" alisema Mangula.
Alisema mapambio, chereko chereko na watu wengi katika mikutano ya kampeni hayawezi kuongeza idadi ya wapiga kura kama hakuna elimu hiyo ambapo aliongelea umuhimu wa mabalozi wa nyumba kumi katika upigaji wa kura kuwa ni watu muhimu sana kwa vile wanawajua watu wao na kuweza kuwahamasisha kwenda kupiga kura.
Mangula akitumia hafla hiyo kumkabidhi mbunge huyo mteule Miraji Mtaturu ilani ya uchaguzi ya chama hicho ya mwaka 2015/2020 ikiwa ni ishara ya kuanza kazi ya kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo la Singida Mashariki.
Mtaturu akitoa shukurani kwa wana CCM hao alisema atashirikiana nao kwa dhati na kuhakikisha jimbo hilo linakuwa na maendeleo ambayo waliyakosa kwa kipindi cha miaka tisa kwa kile alichoeleza halikuwa na mbunge sahihi wa kuwatumikia na sasa Singida imekuwa ni ya kijani.
No comments:
Post a Comment