Dk. Agnes Kijazi (katikati) akichangia mjadala wa usawa wa jinsia (Implementation of WMO Gender Equality Policy and Action Plan) kwenye mkutano wa 18 wa WMO unaoendelea jijini Geneva, Uswisi. |
“TUNAOMBA WMO iweke miongozo maalumu ya usawa wa jinsi katika utekelezaji wa majukumu ya utoaji huduma za hali ya hewa ili nchi wanachama waweze kuwa na utaratibu wa pamoja kwenye utekelezaji wake hususan kwa wanawake,” alisema Dk. Agnes Kijazi.
Dk. Agnes Kijazi ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa
Tanzania (TMA) na mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Shirika la Hali ya
Hewa Duniani (WMO) ambaye kwa sasa anagombe nafasi ya umakamu wa tatu wa Rais
wa WMO alisema hayo wakati akichangia mjadala wa usawa wa jinsia
(Implementation of WMO Gender Equality Policy and Action Plan) kwenye mkutano
wa 18 wa WMO unaoendelea jijini Geneva, Uswisi.
Vilevile, Dk. Kijazi alielezea namna Tanzania kupitia TMA inavyoendelea
kupiga hatua kuhakikisha usawa wa jinsia unazingatiwa kwa wanawake wenye
utaalamu wa sayansi ya hali ya hewa kwakuongezewa ujuzi (mafunzo), kushiriki
katika kutoa utaalamu katika kamati za kikanda na kimataifa hasa suala la
ushiriki wao katika makongamano na warsha mbalimbali.
Aliongezea kwa kusema, TMA imeweka miongozo mbalimbali ya kuwawezesha
wanawake wenye sifa kupata nafasi za uongozi, hivyo kusaidia kuonesha uwezo wa
wanawake katika utekelezaji wa majukumu wanayopatiwa. sambamba na kupata fursa
ya kupaza sauti juu ya umuhimu wa usawa wa jinsia kwa kuwa mfano kwa taasisi za
hali ya hewa Afrika na duniani kwa ujumla.
Dk. Kijazi alitoa mfano wa ushiriki wa wanawake wa TMA katika Mkutano wa 50
wa Kikanda wa Nchi za Pembe ya Afrika (GHACOF-50) unaokusanya wadau kutoka nchi
10 za Pembe ya Afrika ili kuandaa utabiri wa msimu uliofanyika Rwanda ambao
ulienda sambamba na kongamano lililohusu utoaji wa huduma za hali ya hewa zinazolenga
mahitaji maalumu ya wanawake.
Tanzania ilipongezwa kwa kubadilishana uzoefu na nchi zingine wanachama wa
Shirika la Hali ya Hewa Duniani kwa kuonesha jitihada zake za kusimamia usawa
wa jinsia
No comments:
Post a Comment